Kurasa

Jumanne, 20 Septemba 2016

Breaking News: Mabasi yagongana uso kwa uso

Basi la Kampuni ya MANING NICE limegongana uso kwa uso na Basi la HOPE SAFARI katika eneo la karibu na Daraja la Mang'ula Baada Dereva wa Basi la Maning Nice kushindwa kulimudu Basi hilo na kusababisha kugongana Uso kwa Uso na basi la HOPE SAFARI.

MUHANGA WA AJALI HIYO AKISIMULIA.
Baada ya Basi la Hope Safari kuvuka Daraja la Mang'ula ikitokea Morogoro ikipita kibao cha shule ya mlimani ikielekea ifakara ghafla mbele tukaona basi la Maning Nice inashuka ikiwa inaelekea Dar na wakati huo ikiwa imejaa upande wa pili alikotakiwa kupita huyu waliyekuwa wanapishana naye na kwa sababu Maning alikuwa na spidi kali hakuweza kusovu tatizo na ndipo Mabasi yote mawili yakagongana uso kwa uso upande wa abiria baazi wamepata majeraha isipokuwa madreva wote wawili wameumia sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni