Kurasa

Jumanne, 13 Septemba 2016

Polisi wawatambua magaidi 2 wa kike walioshambulia kituo cha Mombasa

 Kenia Mombasa Angriff auf Polizeistation

Polisi nchini Kenya wamewatambua watu wawili miongoni mwa washambulizi watatu wa kike waliouwawa,baada ya mpango wao wa kufanya mashambulizi dhidi ya kituo kikuu cha polisi mjini Mombasa kutibuliwa

Wanawake hao wawili ambao ni raia wa Kenya ni Tasnim Farah na Fatuma Omar. Wenzao watatu wanazuiliwa na polisi kusaidia katika uchunguzi baada ya kufuatiliwa hadi eneo la kibokoni Mombasa. Nilizungumza na mchambuzi wa maswala ya usalama nchini Kenya Mwenda Mbijiwe na kwanza anaeleza hali jumla ya usalama Mombasa kufuatia shambulizi hilo.
Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:Jane Nyingi
Mhariri:Yusuf Saumu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni