
Ndege mbili za
kivita za Marekani zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia B-1 Lancer
zimepaa juu ya anga ya Korea Kusini, siku chache baada ya Korea
Kaskazini kufanya jaribio la tano la silaha za nyuklia.
Ndege hizo
zilipaa si mbali sana kutoka ardhini juu ya kituo cha kijeshi
kinachopatikana kilomita 77 kutoka mpaka wa Korea Kaskazini na Korea
Kusini.Marekani imeitahadharisha Korea Kaskazini kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya taifa hilo baada ya kufanyika kwa majaribio hayo ya bomu Ijumaa.
- Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini
- Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
- Korea Kaskazini yashutumiwa kwa kulipua bomu
'Ndege aina ya B-1 zina uwezo wa kubeba makombora yenye mabomu ya nyuklia au mabomu ya nyuklia yenyewe yenye uwezo wa kuharibu hata mahandaki.

Kamanda wa jeshi la Marekani eneo la Korea Jenerali Vincent Brooks (pili kutoka kulia) amesema hatua ya Pyongyang imezidisha hali ya wasiwasi eneo hilo
Operesheni hiyo ya kupaa kwa ndege ilikuwa imepangiwa kufanyika Jumatatu lakini ikacheleweshwa kutokana na hali mbaya ya hewa Guam, eneo ambalo ndege hizo hukaa.
Chanzo bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni