ILIPOISHIA
“Hakikisheni huyu dada nina lala naye usiku wa leo sawa”
Muntar
aliwaamrisha wapambe wake na wakamtii na mmoja wao akanyanyuka kwenda
kumfatwa Agnes kwenye eneo la kuuzi vinywaji ili kuzungumza ombi la bosi
wake analo lihitaji
ENDELEA
“Habari yako dada?”
Kijana
wa Muntar alimsalima Agnes ambaya kwa haraka akaliachia tabasamu lake
mdomoni na kuufanya uso wake kuzidi kunawiri kwa uzuri
“Salama mamo vipi?” Agnes alizungumza kwa sauti nyororo ya kuvutia hadi muhudumu kiume wa vinywaji akaguna
“Salama.....kwa jina mimi ninaitwa Kibopa na yule pale alavalia cheni nyingi ni bosi wangu anaitwa Muntari”
“Aahaa nashukuru kuwafahamu,Samahani kaka ninaomba unipatie Red’s mbili za baridi kiasi”
“Muhudumu mpe katon nzima pesa nitalipa mimi?”
“Jamani kaka yangu mimi sio mnywaji sana”
“Ahaa usijali nyingine unaweza kunywa leo au hata kesho”
“Asante sana”
Muhudumu akamkabidhi Agnes katoni ya kinywaji alicho muagizia na kibopa akatoa pesa na kumlipia muhudumu.
“Sasa sister kama huto jali ninaomba namba yako ya simu”
Agnes bila wasiwasi akamtajia Kibopa namba yake ya simu,wakaagana ana Agnes akarudi sehemu alipo Rahab
“Jamaa ameshaingia mkenge sasa kazi ni moja sawa”
“Hapo ndipo ninakupendea Ag”
“Chezea mimi wewe,kumbe mtu ukiwa na kalio kubwa nalo linasaidia”
Wakacheka
na kufungua vinywaji na kuanza kunywa taratibu.Muntar akakabidhiwa
namba na Kibopa na akaipiga na Agenes akaipokea na kama kawaida na sauti
yake nyororo aliyobarikiwa kutoka mbinguni akazungumza
“Nani mwenzangu?”
“Ukigeuka upande wako wa kushoto utaniona nimevaa shati jeupe na cheni za dhahabu”
Agnes akageuka na kumfanya Muntar kupunga mkono akimuashiria kuwa ni yeye ndiye aliye mpigia simu
“Mrembo nakuomba basi uje kujumuika name hapa?”
“Naona aibu labda nije na mwezangu”
“Hilo tuu hakuna tatizo ni wewe tuu”
“Sawa ninakuja”
Agnes
akakata simu na kumtazama Rahab kwa pamoja wakatabasamu na wakasimama
na kuanza kutembea kwa mwendo wa maringo na kupishwaviti na wapambe wa
Muntar kisha wakakaa
***
Dokta
Wiliama akawashusha kwenye gari Anna,Halima na Fety mbali kidogo na
hotel ya Serena huku kila mmoja simu yake ikiwa na salio la kutosha
pamoja na picha ya Karim Yussuf kijana mwenye umri mdogo ila anasifika
sana kuwa na utajiri mkubwa kutokana na Sheli za mafuta anazo zimiliki
kila kona ya mikoa ya Tanzania.Kila mmoja akaingia Hotelini kwa muda
wake na kuelekea kuketi katika upande wake ila kwa pamoja wakawa na
mawasiliano ya ujumbe mfupi wa meseji.Kutokana ni muda wa jioni hawakuwa
na papara kwani watu wengi bado hawakuwa wameingia Hotelini kuendelea
na starehe zao.Macho ya Fety yakatua kwa jamaa anayeingia kwenye mlango
wa kuingilia akiwa ameongozana na mwanamke mrembo
{Nimemuona}
Fety
akausamba ujumbe kwa wezake ambao wapo maeneo ya tofauti kwenye hoteli
na taratibu simu yake akaichomeka kwenye suruali yake na kuendelea
kumtazama Karim ambaye moja kwa moja aka anaelekea sehemu yenye milango
ya lifti zinazo kwenda juu na kushuka chini,Kutokan-a na Lifti kutumika
ikamlazimu Karimu na mpenzi wake kusimama kwa muda kuzisubiria.Kwa
haraka Fety akasimama na kupiga hatua za haraka kabla hajafika sehemu
alipo Karimu,lifti ambayo wanaisubiria ikafunguaka,Karim na mpenzi wake
wakingia ila kabla haijajifunga Fety akawahi kuizuia na kuingia
“Habari zenu?”
“Salma”
Karimu
kutokana na kutokuwa na aibu akaanza kumshika shika mpenzi wake na
kuchezeana katika sehemu zao nyeti.Mcho ya Fety yakawangalia kwa umakini
kisha akayahamishia masho yake kwenye kamera mbili za ulinzi zilizopo
ndani ya lifti kabla hajafanya kitu chochote akastukia lifti ikisimama
hii ni baada ya mpenzi wa Karimu kuminya kitufe cha kuisimamisha
lifti.Kufuma na kufumbua Fety akastukia ngumi kutoka kwa mpenzi wa Karim
ikitua kwenye shavu lake na kumsfanya kuweweseka kasha akaanza kuikwepa
mikono inayoimjia mwilini mwake kutoka kwa Karimu na mpenzi wake Shamsa
mwenye asili ya kiarabu.
**
Karimu
na Shamsa wanaasili ya Oman japo wanauraia wa nchi zote mbili Tanzania
na Oman,japo watu wengi waliwaona machoni mwao wanadhani ni watu wema
hii ni kutokana na jinsi wanavyo jitoa katika shughuli mbali mbali za
kijamii na mara nyingi huwa wanawasaidia wasio jiweza kila siku ya
Ijumaa na jumamosi nje ya jumba lao lililopo maeneo ya Mbezi beach.Japo
wanautajri mkubwa wa magari ya kifahari,masheli,maduka na mahoteli ya
kifahari ila bado hawaridhiki na utajiri huo na wanaendelea kufanya
kazi za haramu ili kuzidi kuuongeza utajiri mara dufu.Jambo la kuua kwao
ni sawa na mtu kumchinja kuku siku ya sikuku.
Hadi
wakati huu Serikali ya Tanzania inashindwa kutambua ni jinsi gani
wanaweza kuwatia nguvuni Karimu na mpenzi wake wakiwa katika
kidhibitisho kitakacho wawezesha kuwastaki katika mahakama kuu ya
Tanzania na kuwatupilia jela.Kila mbinu ambazo serikali waliitumia
wakajikuta wakishindwa hii ni baadhi ya viongozi wasio waaminifu
kuwapenyezea siri Karim na Shamsa na hujipanga upya katika kuwatoroka
askari.
Amri ya kuwaua watu waote wanaoshindikana kukamatika na kirahisi ilitolewa ma raisi tena kwa siri kubwa na watu walio husishwa katika kazi hiyo ni Dokta William na Mkuu mstaafu wa jeshi bwana Clinton Tony ambao wote ni miongoni mwa watu wa karibu sana wa raisi na mara nyingi humshauri riasi katika maswala mengi ya kukabiliana na ugaidi hii ni kutokana na ujuzi wao katika maswala ya kigaidi
Amri ya kuwaua watu waote wanaoshindikana kukamatika na kirahisi ilitolewa ma raisi tena kwa siri kubwa na watu walio husishwa katika kazi hiyo ni Dokta William na Mkuu mstaafu wa jeshi bwana Clinton Tony ambao wote ni miongoni mwa watu wa karibu sana wa raisi na mara nyingi humshauri riasi katika maswala mengi ya kukabiliana na ugaidi hii ni kutokana na ujuzi wao katika maswala ya kigaidi
Pasipo
wao kujua Agnes,Anna,Rahab,Fetty na Halima wanatumiwa na serikali
kisiri na kwaimani yao wanatambua kuwa mtu anaye waagiza kazi hiyo ni
dokta Williama ambaye amewafundisha mbinu nyingi za kigadi ili kupambana
na magaidi wanao itesa serikali ya Tanzania pamoja na jeshi la polisi.
***********
Fetty
anajipanga vizuri na kuanza kupambana nao kufa na kupona kutokana na
ujuzi mkubwa wa kukabiliana na adui anafanikiwa kumpiga Shamsa ngumi
kadhaa sehemu ya shingo na kumfanya apate wenge linalo mkalisha chini
huku machoni mwake akiona nyota nyota nyingi.Karimu anashangaa kukutana
na msichana jasiri anaye vumilia makonde ya mazito kutoka kwake na kwa
haraka anamisha kitufe na lifti inaanza kwenda juu huku akiendelelea
kuyapangua mateke ya Fetty kwa kutimia mikono yake iliyo komaa.
Lifti inafunguka gorofa ya tano na Karimu anajirusha nje kabla Fetty hajapiga hatua anastukia akishikwa mguu na kuvutwa chini na Shamsa na kuangukia uso na kumshuhudia Karimu akichanganya miguu kwa kasi kubwa na kupolelea anapo pajua mwenyewe.Shamsa akamkalia kwa haraka Fetty mongoni na kuanza kumvuta nywele huku akijaribu kukipigisha kichwa cha Fetty chini.Kwa nguvu zake zote Fetty akajikaza mwili wake kuanzia juu hadi chini na kujinyanyua kwa nguvu hadi akasimama ila Shamsa akaendelea kumng’angania mgongoni huku mkono wake ukiwa umeikaba kwa nguvu zake zote shingo ya Fetty.
Lifti inafunguka gorofa ya tano na Karimu anajirusha nje kabla Fetty hajapiga hatua anastukia akishikwa mguu na kuvutwa chini na Shamsa na kuangukia uso na kumshuhudia Karimu akichanganya miguu kwa kasi kubwa na kupolelea anapo pajua mwenyewe.Shamsa akamkalia kwa haraka Fetty mongoni na kuanza kumvuta nywele huku akijaribu kukipigisha kichwa cha Fetty chini.Kwa nguvu zake zote Fetty akajikaza mwili wake kuanzia juu hadi chini na kujinyanyua kwa nguvu hadi akasimama ila Shamsa akaendelea kumng’angania mgongoni huku mkono wake ukiwa umeikaba kwa nguvu zake zote shingo ya Fetty.
***
Simu
za Fetty,Halima na Anna zina Software ambayo kila mmoja wao anapo
kwenda ni lazima simu zao ziingize ujumbe katika simu za wezao kuwa ni
sehemu gani alipo mmoja wao.Anna akampigia simu Halima na kumpa taarifa
Anna wakutate katika milango ya kiingilia kwenye lifti
“Anna,Fety
yupo kwenye matatizo ninavyohisi kama unaweza kuiona simu yako
inavyoonyesha kuwa yupo eneo maoja tuu kwa zaidi ya dakika kumi sasa”
“Location inaonyesha yupo gorofa namba tano”
“Sasa tujigawe,wewe pita kwenye ngazi na mimi nitumie lifti”
“Sawa”
Halima
akaingia kwenye lifti na kuminya kitufe cha gorofa ya tano,huku alima
naye akaanza kuzipandisha ngazi kwa haraka kuelekea juu gorofa ya tano
japo ni ndefi ila akajikata kutembea kwa mwendo wa kukimbia
***
Kwa
haraka wazo lililo mjia Karimu ni kushuka kwa kupitia ngazi kuepukana
na kukutana na Fetty ambaye tayari alisha mzidi ujanja na maarifa ya
kila aina.Karimu akaanza kushusha kwenye ngazi huku akikimbia na
kutazama tazama juu kama Fetty akamfwata ajue ni jinsi gani ya kuongeza
juhudi za kukimbia.Macho ya Anna yakamshuhudia jinsi Karimu anavyoshuka
kwa kasi huku hasho jingi likimwagika na shati lake likiwa limejikunja
kunja kama limetafunwa na ng’ombe mwenye njaa kali,Anna akapunguza
mwendo na hadi Karimu anamfikia kwa ustadi mkubwa wa hali ya juu
akampiga teke la miguu Karimu na kumfanya aanguke vibaya na kuanza
kubingiria kwenye ngazi akielekaea chini akitoa kelele kali za vilio.
***
Fetty
akaanza kuishiwa na pumzi mwilini mwake kutokana na kabali takatifu
aaliyo pigwa na Shamsa msichana ambeye kwenye maeneo mazima ya kupiga
anayapenda tangu akiwa mtoto mdogo wa miaka mitano.Fetty kila alipo
jaribu kuitoa mikono ya Shamsa akajikuta akishindwa kwani Shamsa
anahakikisha kuwa anaondoka na roho ya Fetty,taratibu Fetty akaanza
kushuka chini huku jicho likiwa linaanza kumtoka akimshuhudia mtoa roo
akiinyemelea roho yake.Mlango wa lift aliyo panda Halima ukafunguka na
akatoka nje akatazama pande zote za kardo akaona hakuna dalili yoyote na
mtu,Akasikia kishindo na kukuroma kwa mtu kwenye mlango wa pili wa
lifti ambao unshindwa kujifunga kutokana na kiatu chekundu lilicho zuia
katikati na kuifanya milango hiyo kujisogeza na kurudi inapotoka.Halima
akamshuhudia Fatty akilazwa chini na msichana anaye miminika kwa jasho
jingi japo ndani ya lifti hii kuna hewa ya kutengenezwa AC(air condion)
Halima
hakupoteza muda,akaingia na kuzishika nywele za Shamsa na kumvuta nje
kwa nguvu zake nje na kumfanya Shamsa kuburuzika kwenye sakafu
iliyotengenezwa vizuri na kufanania na kioo.Akamgauza Faetty na kumkuta
akikohoa kohoa akiyaruhusu mapafu yake kuingiza hewa ya kutosha.Shamsa
akasimama na kuanza kukimbia kujiokoa maisha yake
“A....nak....imbi....a.”
Fetty alizungumza kwa shida huku mkono wake mmoja akimnyooshea Shmsa anayechanja mbuga
“Upo vizuri lakini?”
“Nd...io muwah....i anatoroka”
Halima
akamtazama vizuri Fetty na kuridhishwa na afya yake na akasimama kwa
haraka na kuanza kumkimbiza Shamsa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya
kukimbilia zaidi ya kujirusha kwenye mlango mmoja uliopo mbele yake na
kwabahati nzuri mtu aliyopo ndani ya chumba hicho ndio alikuwa
ameufungua na kukishika kitasa cha mlango wake kwa ajili ya kutoka nje.
Kikumbo cha Shamsa kikamfanya mwenye chumba kuanguka chini pamoja na simu yake ambayo alikuwa anasoma meseji iliyomfanya asimame kwenye mlango huku akiwa ameshika kitasa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya bafuni ambapo Halima naye akaingia na kwa haraka Shamsa akachukua kibakuli chenye sabuni ya unga na kumbwagia Halima ya uso
Kikumbo cha Shamsa kikamfanya mwenye chumba kuanguka chini pamoja na simu yake ambayo alikuwa anasoma meseji iliyomfanya asimame kwenye mlango huku akiwa ameshika kitasa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya bafuni ambapo Halima naye akaingia na kwa haraka Shamsa akachukua kibakuli chenye sabuni ya unga na kumbwagia Halima ya uso
***
Muntar na watu wake wakazidi kunywa pombe na kuwaomba Agnes na Rahabu wawe wageni wao kwa usiku wa leo.
“Jamani
sisi hatuhitaji kulala kwenye hoteli hii.” Agnes alizungumza huku
akikichezea kifua cha Muntar ambaye muda wote anakazi ya kutabasamu
tabasamu
“Nyinyi mutanata wapi watoto wazuri?”
“Hoteli yoyote ila si hapa”
“Wee kibopa fanya mpango wa kutafuta vyumba vya mjini kwenye hoteli nzuri nzuri unazo zijua”
“Bosi hotel ambayo ipo powa kwa haraka haraka ninaona ni Mtendele”
“Ipo wapi hiyo?”
“Maeneo ya Chuda raha”
“Sawa twendeni”
Wakasimama
na wote wakatoka nje,Rahabu na Agnes wakaingia kwenye gari lao na
Muntar na wapambe wake wakingia kwenye gari yao aina ya HAICE na
taratibu wakaanza safari ya kuelekea katika Hotel ya Mtendele
“Ag hawa watu tunawaua kwa nama gani?”
“Una maana gani?”
“Namaanisha kwa kuwanyonga au kwa kuwapiga risasi?”
“Lengo letu sisi ni huyo Muntar hao wengine tuwapotezee”
“Huoni watakuwa ni watu wa kwanza katika kutusaka sisi?”
“Sawa ila tutajua ni jinsi gani ya kuwaua endepo nao wataingia kwenye kumi na nane zetu”
“Powa hii ishu tuifanye usiku huu huu na turudi zetu kambini”
“Powa ni wewe tuu kikubwa ni umakini na hiyo bastola yako ikoki tayari kwa mashambulizi”
***
Muntar na wapambe wake wanaendelea kuburudika na mziki gafla Muntar akazima redio ya gari na kuwafanya wapambe wake kumtazama
“Sikilizeni nyinyi....mpango wetu ni kama munavyo ujua,Sisi mwanamke kwetu ni begi la safari na hawa pia iwe hiyo hivyo”
“Sawa bosi ila mimi sijaelewa kidogo hapo kwa maana hawa nao pia tunatakiwa kuwaua?”
“Ndio ni lazima wafe”
“Ahaaa bosi huoni maduu wazuri kama hawa pia tuwauee ,Acha basi tuspend nao kama siku mbili tatu nne hivi”
Kwa haraka Muntar akachomoa bastola yeka na kumelekezea Kibopa ambaye muda mwingi anapenda sana wasichana wazuri
“Katika
wakati wa kazi huwa sipendi masihara.....na ole wenu miongoni mwenu
nione mtu anajipendekeza kwa msichana yoyote nitamtoa roho,Tuna wakamata
na kuwachinja na ndani ya matumbo yao tunadumbukiza shehena yote ya
madawa ya kulevya tuliyo nayo.SAWA?”
“Sawa bosi’
Wote
wakaitikia kwa woga huku Kibopa mwili wake wote ukiwa unamtetemeka
kwani Muntar ni mwanaume asiye na huruma kwa mtu wa aina yoyote katika
swala zima la biashara zake haramu.Usemi wake mkubwa ni bora punda afe
ili mzigo ufike
SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……4
Kwa
bahati mbaya katika maeneo ya barabara ya Railys,wakakuta ajali ya
daladala iliyosababisha magari mengi kusimama kwa muda,Kutokana hawakuwa
na haraka ikawalazimu kupanga foleni na kuwaacha askari wa usalama
barabarani kumaiza vipimbo vyao.
“Rahab nahisi kuna kitu kwenye gari la kina Muntar.” Agnes alimuambia Rahabu
“Kitu gani?”
“Kama
wanakitu wanakijadili na ona oana jinsi Muntar anavyo zungumza huku
akiichezesha chezasha mkono wake ulioshika bastola?” Agens alimuonyesha
Rahab na kwakusaidiwa na mwanga wa taa za magari mengine waliweza
kuliona tukio la ndani ya gari
Rahab akaitoa bastola yake na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti,akataka kushuka kwenye gari ila Agnes akamzuia
“Mbona unakuwa kama mjinga unataka kwenda wapi?”
“Tuwafyatue tusepe zetu”
“Huoni hao askari hapo au unataka tukimbizane kimbizane?”
Wote wakajikuta macho yao yakimsindikiza askari anaye gongwa kwenye kioo cha gari walilomo Muntar na watu wake
***
Muntar akamtazama askari anaye gonga kioo cha gari lao,Akaitazama astola yake na kukishusha kioo taratibu
“Shukeni
ndani ya gari.” Askari aliwaamrisha na kuwamfaya Muntar kufyatua risasi
mbili kwa haraka,milio ya risasi ikawafanya watu waliopo kwenye eneo
kuanza kutawanyika kuokoa maisha yao.Askari wengine watatu waliopo
katika eneo la tukio wakajibanza kwenye magari mengine wakiwa na bunduki
zako na kuanza kujibu mashambulizi kuelekea kwenye gari la Muntar
“Rudisha nyuma gai hilo.”
Muntar
alimuamuru dereva wake na akatii,Wakaligonga gari walilomo Agnes na
Rahab na kulifanya lirudi nyuma na kuyagonga magari yaliyopo nyuma
yetu.Rahab akaanza akaanza kufyatua risasi katika matairi ya gari la
Muntar na kulifanya lipoteze muoelekeo hii ni baada ya breki za gari lao
kushindwa kukamata vizuri na kugonga kwenye vyuma vya reli.Watu wa
Muntari,mmoja baada ya mwengine wakaanza kujirusha nje ya gari wakiwa na
bunduki zao aina ya ‘Short gun’ na kuendelea kufanya mashambuliza kwa
askari.
Agnes
akafungua mlango wa gari lao na kupiga goti moja chini,Bastola yake
ikawa na kazi mija tuu ambayo ni kufyatua risasi kwa kila mtu wa
Muntar.Muntar akazidi kuchanganyikiwa baada ya watu wake kuwaona wakiwa
wanaanguka mmoja baada ya mwengine.Hadi akabaki akiwa na Kibopa ambaye
wakati wote wezake wakipambana yeye alikuwa na kazi ya kujibanza kwenye
gari lao
Muntar
akaona nafasi pekee ni kukimbia,kwa bahati nzuri pembeni kuna pikipiki
iliyo acha na raia aliyekuwa akijiokoa maisha yake kwa kuiamini sana
miguu yake kuliko pikipiki.Akapanda na Kibopa akadanda kwa nyuma
wakaondoka kwa kasi wakikatiza katokati ya njia za reli.
Agnes
na Rahab wakaingia ndani ya gari,Agnes akalirudisha gari lao nyuma na
kupata upenyo wa kuiwezesha gari yao kupita na kupita njia ambayo Muntar
amekimbilia.Askari wakashindwa kufyatua risasi kwatika gari linalo
wafukuzia majambazi kwani hawakujua walio wasaidia ni kina nani.
Muntar
akazidi kukanyaga mafuta na kuingia barabara inayokwenda mikoani
akikatiza katika kiplefti cha kwaminchi,Agnes akawa na gazi ya kupiga
honi akiashiria watu waliopo barabarani kuwapiasha.Akazidi kukanyaga
mafuta kwa kasi huku akiikaribia pikipiki ya Muntar.Kibopa akaanza
kufyatu risasi kuelekea lilipi gari walilopo Agens.
“Shiti....”
Rahab alizungumza huku akinang’ata meno yake,alikataka kujitokeza
kwenye kioo cha gari ila akarudi ndani kwa haraka baada ya kioo kidogo
cha pembeni kuvunjwa kwa risasi anazo zipiga Kibopa pasipo kuwa na
utaratibu wowote.Gafla kibopa akalikwepa Scania linalo toka kwenye
kiwanda cha unga Pembe maeneo ya Kange na karibia robo mbili ya gari
imeziba barabara na kuachanisha uwazi mdogo unao weza kuiruhusu pikipiki
kupi na kuendelea mbele kwa kasi.Agnes akafunga breki za gari lake kwa
kasi na kuiingiza upande wa kulia kwake kukikwepa kichwa cha gari kubwa
la unga,Gari karerereka pembeni ya barabara na kwakusadiana na Rahab
wakaushika mskani wa gari na kuurudisha upande wa kulia
Gari
ikakaa sawa barabarani,kutokana na mstuko katika injini,gari ikazima
katikati ya barabara na milago yote kujifunga.Kwa kutumia vitako vya
bastola zao wakapasua vioo vya madirisha ya magari na kujitoa ndani ya
gari lao,linalo toa mlio wa kuashiria linaitilafu sehemu
“R...itakuwaje sasa?”
“Ndio hivyo jamaa wamesha sepa.”
“Ngoja kwanza.” Agnes akaenda eneo lenye maegesho ya boda boda(waendesha pikipiki),
“Ni kina nani wanaweza kuendesha pikipiki kwa kasi kubbwa?”
Kila muendesha pikipiki akaa kimya huku macho yao wakiitazama bastola ya Agnes.
“Ohoo nahisi munaiogopa hii bastola? Mimi ni raia mwema ninaomba masaada wa kuwakimbiza wale watu walio pita hapa?”
”Dada
mimi piki piki yangu haina mafuta?” Jamaa mmoja alizungumza huku
akilivua kofia lake,wengine wote wakakataa.Rahab akafika eneo alipo
Agnes
“Ag wanasemaje?”
“Hawataki?”
Rahab
akapiga risasi moja hewani,kila dereva aliye ipenda rogo yake akaaruka
kwenye pikipiki yake na kuchanganya kwato zake kuooa maisha yake.Rahabu
akapanda kwenye moja ya piki piki aina ya Boxer,ambayo dereva wake
aliisahau funguo yeke.Muntar kadri anavyozidi kuendesha pikipiki ndivyo
jinsi mafuta yaliyozidi kuteketea,na taratibu piki piki ikaanza kugoma
na mwisho wa siku ikagoma kabisa hata kusogea hatua mbele.Rahab akazidi
kuvuta mafuta ya pikipiki waliyo panda,kwa mbali wakawaoana Muntari na
Kibopa wakishuka kwenye pikipiki yao na kuinga pori.
***
Shamsa
baada ya kumuona Halima anaanza kuhangaika kwa sabuni ya unga aliyo
mwagia usoni,kwa haraka akafungu mlango wa chumba na kuaanza kukimbia
kuelekea zilipo ngazi za kushuka.
Anna
kwa haraka akashuka kwenye ngazi na kuanza kumshindilia mateke Karim
ambaye amechoka kwa kiasi kikubwa sana.Karim akajihahidi kujiinua ila
Anna akawa makini kwa kila jambo na kwa haraka akaiwahi shingo ya Karimu
na kuizungusha kwa nguvu na kuivunja.Kitendo cha Karimu kuuawa
kikashuhudiwa na Shamsa ambaye ndio yupo kwenye harakati za kujiokoa
kutoka mikononi mwa Halima.
Anna
hakumjali Shamsa ambaye amesimama kwa mshangao akiwa haamini kwa kitu
kilicho tokea kwa mpenzi wake anaye mpenda kuliko kitu cha aina
yoyote.Kwa haraka Shamsa akashuka kwenye ngazi kwa hasira na kumrukia
Anna ambaye akajibamiza kwenye ukuta,Shemsa akajaribu kumrukia Anna
ambaye alifanikiwa kumkwepa na kwa bahati mbaya Anna akamsukuma Shamsa
ambaye akaanza kwenda chini kutoka gorofa ya nne hadi kwenye sakafu na
kichwa chake kikapiga chini na kikapasuka mbele ya macho ya polisi na
baadhi ya wateja wengine
Anna
taratibu akapiga hatua na kuchungulia sehemu aliyo angukia macho yake
yakakutana na askari tishio ambaye ni mpelelezi wa kutegemewa nchini
bwana Jackson Luther
***
Rahab
anazidi kuvuta mafuta ya pikipiki hadi kwenye njia walio ingilia Muntar
na KIbopa mbao walizidi kuongeza mwendo wa kukimbia baada ya kuiona
pikipiki ikiwafwata kwa kasi nyuma yao.Kwa bahati mbaya Muntar na
Kibopa waliishiwa risasi katika silaha zao,kila mmoja akakimbia kwa
upande wake anao ujua yeye ili kutaokoa maisha yake,Rahabu akapunguza
mwendo wa pikiki na Agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda
Kibopa,Rahab akapita njia aliyo kwenda Muntar.
Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla Rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na Muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi
Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla Rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na Muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi
ITAENDELEA....
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni