Kurasa

Jumamosi, 17 Septemba 2016

Al Shabab waondoka mji wa El Wak

Bado Al Shabab wanadhibiti maeneo makubwa kusini na kati kati mwa Somalia
Bado Al Shabab wanadhibiti maeneo makubwa kusini na kati kati mwa Somalia

Kundi la wanamgambo la Al Shabab limeondoka kutoka mji ulio Kusini Magharibi mwa Somalia ambao liliuteka baada ya mapigano makali siku ya Ijumaa.

Takriban watu sita waliuawa wakati wa mashambulizi yaliyotokea mji wa El Wak wakiwemo wanajeshi wawili.

Baada ya Al Shabab kuondoka, jeshi la Somalia lilingia mjini humo.

Licha wa kutimuliwa kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011, Al Shabab bado wanadhibiti maeneo makubwa ya Kusini na kati kati mwa nchi na lina uwezo wa kufanya mashambulizi kwingine.
Chanzo:bbcwahili.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni