Kurasa

Jumanne, 13 Septemba 2016

Viongozi wa dini UK, walia na sheria ya uhamiaji

 
Zaidi ya viongozi 200 wa dini tofauti nchini Uingereza wameitaka serikali ya nchi hiyo kulegeza sheria za uhamiaji kwa wahamiaji kutoka nchini Syria na maeneo mengine ili waweze kuungana na familia zao.

Katika barua viongozi hao waliyomwandikia waziri mkuu, wamesema ndugu wa karibu wa Waingereza na wakimbizi ambao nchini humo wanaishi ugenini katika hali ya mashaka na wanatakiwa kupewa njia halali ya kuingia nchini humo.

Wamesema wahamiaji hao wamekuwa wakisafiri katika safari hatarishi.
Askofu Mkuu wa zamani wa Canterbury Rowan Williams ni mmoja wa wakilishi kutoka viongozi hao wa dini waliokutana wakitoka katika madhehebu ya Buddhist, Wakristo, Wayahudi, Wahindu, Waislamu na imani ya Sikh ambao walisaini barua kwenda kwa waziri Mkuu Theresa May.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni