Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema ikiwa waamuzi
hawatazingatia kanuni na taratibu katika uchezeshaji, huenda ladha ya
ligi ikapungua.
“Waamuzi wanapaswa kuwa makini muda wote kwa kuchezesha soka kwa
kuzingatia kanuni na taratibu, inapunguza ladha unapoona mwamuzi
alitakiwa kutoa adhabu katika eneo fulani lakini anaminya,” amesema
Pluijm baada ya kushuhudia mwamuzi Ahmed Seif aliyechezesha mechi kati
ya Mbao FC na African Lyon akitoa uamuzi wenye utata.
Mjumbe wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Jamal Rwambow licha ya
kukiri ligi ya msimu huu itakuwa na ushindani mkubwa ameonyesha wasiwasi
wake kwa waamuzi akidai huenda wakachangia kuvuruga ligi hiyo.
“Niwe muwazi, ligi ni nzuri na yenye ushindani. Unaona timu zimesajili
na zinapambana kusaka matokeo katika kila mchezo. Wasiwasi wangu uko kwa
waamuzi, maana tunaweza kuwa na ligi nzuri lakini waamuzi wakatuangusha
kwa kutofuata kanuni na taratibu,” amesema Rwambow ambaye ni ofisa
mstaafu wa Jeshi la Polisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni