Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney hajajumuishwa
katika kikosi kilichosafiri kwenda Uholanzi kwa ajili ya mechi ya Europa
ligi dhidi ya Feyenoord.
Jose Mourinho akiongea na waandishi wa habari amesema haya kuhusu Wayne Rooney
“Amecheza kila mechi tangu kuanza kwa msimu huu na amecheza dakika 90
katika timu ya Taifa ya England. Ninataka awe vizuri kwa ajili ya mechi
zijazo . Anacheza katika eneo la ushambuliaji ambapo nina machaguo
mengi.”
Wachezaji 20 ambao wameenda Uholanzi ni De Gea,Romero, Johnstone,
Darmian,Bailly,Blind,Mensah,Rojo,Smalling,Carrick,Fellain,Herrera,Mata,Memphis,Pogba,Schneiderlin,Young,Ibrahimovic,
martial Rashford.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni