Kurasa

Alhamisi, 15 Septemba 2016

Mjane wa Aboud Rogo afikishwa kortini Mombasa

Hania Rogo alikamatwa na polisi Jumatano jioni
Hania Rogo alikamatwa na polisi Jumatano jioni

Mjane wa mhubiri wa Kiislamu aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana miaka minne iliyopita amefikishwa mahakamani Mombasa kuhusiana na shambulio lililotekelezwa katika kituo cha polisi Mombasa Jumapili.
Bi Hania Said Saga Rogo alikamatwa Jumatano jioni na maafisa wa usalama.

Taarifa zinasema alikuwa na uhusiano na mmoja wa wanawake watatu waliouawa wakati wa shambulio hilo.
Bi Saga ni mjane wa marehemu Aboud Rogo, ambaye alituhumiwa na vikosi vya usalama vya Kenya na nchi Magharibi kwamba alihusika katika kusaidia watu kujiunga na kundi la al-Shabab nchini Somalia.

Hania Rogo na wakili wake Aboubakar Yusuf kortini Hania Rogo na wakili wake Aboubakar Yusuf kortini

Aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Malindi tarehe 27 Agosti, 2012.

Kuuawa kwake kulisababisha ghasia zilizodumu siku kadha mjini Mombasa. Wakati wa maandamano hayo, guruneti lilirushwa kwenye lori la polisi na kusababisha vifo vya watu wawili.
Chanzo: bbcswahili.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni