Kurasa

Alhamisi, 15 Septemba 2016

Programu ya kuwaleta pamoja majirani yazinduliwa UK

Programu inayowaleta pamoja majirani kwa jina Nextdoor yazinduliwa Uingereza 




 Programu inayowaleta pamoja majirani kwa jina Nextdoor yazinduliwa Uingereza

 

Huduma ya mtandao wa kijamii inayolenga kuwaleta pamoja majirani imezinduliwa nchini Uingereza.
Nextdoor imepata ufanisi mkubwa nchini Marekani na ilizinduliwa nchini Uholanzi mnamo mwezi Februari.
Inalenga kuhamasisha mawasiliano kati ya majirani na kuwafahamisha wakaazi kuhusu visa vya uhalifu.

Mtandao huo tayari umetumiwa na takriban watu 500 nchini Uingereza.
''Kila jirani,atafaidika kutokana mtandao unaorahisisha kuwasiliana na kuzundumza na majirani zao ,alisema Nirav Tolia'',afisa mkuu wa mtandao huo wa Nextdoor.

Pia amefichua kwamba kuondoka kwa Uingereza katika muungano wa Ulaya ni sababu iliofanya Nextdoor kuzinduliwa nchini humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni