Ngorongoro.Watu wanaodhaniwa ni wafugaji wamewauwa mbwamwitu 22
kwa sumu ndani ya eneo la Mamlaka a Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), mkoani
Arusha.
Wakizungumza na waandishi wa habari, mtafiti mwandamizi mradi wa
mbwamwitu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI), Dk
Ernest Mjingo na kaimu mhifadhi Wa NCAA, Julius Kibebe walisema
mbwamwitu hao, wameuawa katika kipindi cha miezi tisa.
Dk Mjingo alisema Septemba 15 mwaka huu wamebaini kuuawa kwa mbwamwitu
11, katika eneo la bonde la Ngutotu katika kijiji cha Kakesyo ndani ya
hifadhi ya Ngorongoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni