Kurasa

Jumatatu, 19 Septemba 2016

Watanzania milioni 39 hawana vyeti vya kuzaliwa

NUKUU “Hali ya usajili wa vizazi nchini hairidhishi. Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 na takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ni asilimia 13 tu ya Watanzania ndiyo wamesajili vizazi. Wengi hawana mwamko hasa kwa maeneo ya vijijini,.” 
Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Emmy Hudson amesema kuna changamoto kubwa katika usajili wa vizazi na vifo kiasi kwamba ni asilimia 13 tu ya Watanzania waliosajili na kupewa vyeti vya kuzaliwa.

Kwa takwimu hizo, ina maana takriban watu 39,088,163 kati ya 44,928,923 waliopo nchini kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2012 sawa na asilimia 87, hawajaandikishwa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Hudson alisema sababu za mifumo ya ukoloni iliyobagua watu katika usajili na Sheria ya Usajili vimechangia hali hiyo.

Alisema kutokana na hali hiyo Tanzania iko nyuma kwa usajili wa vizazi barani Afrika ikifuatiwa na Somalia yenye matatizo ya vita kwa muda mrefu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni