Moja
ya changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara wengi ni kutokujua
kwa undani jinsi ya kufanya utafiti wa kimasoko katika biashara ambayo
anaifanya au anataraji kuifanya, na kutokana na changamoto hiyo, imepelekea biashara nyingi kushindwa kukua na hata kupelekea baadhi ya biashara nyingine kufa kabisa.
Hivyo
ni jambo jema ukayafahamu mambo ya msingi yahusuyo masuala ya masoko
katika kibiashara ili kuweza kukuza biashara yako na hatimaye kupata
faida.
Yafuatayo ndiyo mambo ya msingi ya kuzingatia katika kufachanya uchunguzi wa masoko.
1. Nani atakuwa ni mteja wako?
Hili
ni swali la msingi la kujiuliza. Kwa mfanyabiara yeyote ni lazima aweze
kutafakari kwa makini zaidi ni nani ambaye atanunua bidhaa au huduma
ambayo unaitoa. Katika kujiuliza swali hili ni lazima uweze kumchanganua
mteja wako kwa kuangalia mambo yafutayo;
Uwezo wa kiuchumi kwa wahitaji wa bidhaa au huduma.
Kwa
kutazama uwezo wake wa kifedha ni vyema ukajiuliza je kwa bidhaa au
huduma ambayo ninaiuza mteja wangu ana uwezo wa kununua?. Kwa mfano,
huwezi ukafungua biashara ya ‘supermarket’ maeneo ya vijijini kwani hali
ya maeneo mengi ya vijinini hawana uwezo Wa kuweza kununua bidhaa kwa
kiwango kikubwa ukilinganisha na mjini.
Umri na jinsia.
Ni
vyema ukajiuliza kuhusu watumiaji wa bidhaa au huduma yako kwa
kuangalia uhitaji wa bidhaa yako kwa kujiuliza je, ni umri gani ambao
watatumia zaidi bidhaa yako? Na ni lazima ujiulize ni jinsia gani
watapendelea zaidi kutumia bidhaa yako? Ukipata majibu sahihi ndipo
utakapojua ni biashara gani utaifanya katika eneo husika.
2. Upi ukubwa wa kisoko?
Hili
pia ni suala la msingi la kuweza kuzingatia hususani suala zima la
kufanya biashara yenye ubora na yenye kukua. Watu wengi huwa
hawalizingatii hili na hivyo kupelekea biashara kufa, lakini kujua
ukubwa wa soko huusisha masuala ya uhitaji wa bidhaa au huduma, kufanya
hivi kutakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua uwezo wa kuzalisha kwa
kiwango gani kulingana na uhitaji wa wateja wako.
Soma; Mawazo Muhimu Unayotakiwa Kuwa Nayo Ili Kukuza Biashara Yako.
3. Bei itakuwa ni kiasi gani?
Kwa
mjasiriamali yeyote ni vyema ukajua namna ya kupanga bei katika
biashara yeyote ambayo unaifanya au unataka kufanya, kama utakuwa ni
mdau mzuri wa mtandao huu nilieleza namna ya kuweza kupanga bei katika
biashara yako.
Kwa
harakaharaka nikukumbushe ya kwamba katika upangaji wa bei ni lazima
uangalie uhitaji wa bidhaa, gharama za uzalishaji na uendeshaji na pia
ni lazima uwatazame washindani wenzako wanafanyaje katika biashara
hususani suala zima la kupanga bei.
Soma; Mbinu Bora Za Kupanga Bei Katika Biashara.
4. Namna ya kufikisha huduma/bidhaa kwa walengwa.
Hili
ni jambo muhimu kuweza kulifahamu. Katika biashara yeyote ile kuna njia
mbili za kufikisha huduma au bidhaa kwa wateja. Jambo la kwanza ni
kuweza kufikisha bidhaa moja kwa moja kwa mteja, njia hii humkutanisha
mzalishaji na mteja.
Na
jambo la pili kuweza kufikisha bidhaa kupitia ununuzi rejareja au kwa
jumla, njia hii haimkutanishi mzalishaji na mteja. Mfano mzuri kama
tufanyavyo kununua vitu kwa madukani kwa mangi. Hivyo katika kufanya
utafiti wa kimasoko ni lazima ujue namna na mbinu ambazo zitakufanikisha
kufanya biashara kwa ufanisi hatimaye kupata faida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni