utafiti uliofanyika nchini marekani umebaini kwa kila ndoa mia moja
zinazofungwa, hamsini zinavunjika..hali hii pia hapa africa ni mbaya
sana japokua hakuna tafiti zilizofanyika kuangalia hali halisi ikoje.
kumekua kuna makosa mengi sana yanafanyika kabla ya kuoa au kuolewa,
yaani watu hufikiria sana jinsi gani watakua na furaha siku ya harusi
bila kufikiria itakuaje baada ya harusi. watu hawaangalii hali halisi
ikoje na kupofushwa na yale mapenzi motomoto bila kujua kwamba ni ya
muda tu na ipo siku mapenzi yatapoa na macho yako yatafunguka kuona
ukweli.kikristo ndoa ni pingu ya watu wawili ambayo ukiingia hutakiwi
kutoka huko mpaka kifo chako hata kwa waislam na imani zingine ambazo
zinaruhusu mke zaidi ya mmoja usipokua makini wake zako wote wanne
watakushinda.ndoa ina changmoto nyingi sana lakini baadhi ya changamoto
watu huziona kabla ya ndoa na kuingia nazo kwenye ndoa bila kujua huo
ndio utakua msiba wa maisha yao.yafuatayo ni mambo ya msingi sana
yakuzingatia kabla ya kuingia huko.
mapenzi iwe sababu kuu ya ndoa; kuna watu wengi sana wameingia
kwenye ndoa bila kuzingatia hili... watu wameingia sababu ya kufuata
mali[hasa wanawake], sababu ya presha za familia zao, sababu ya upweke,
sababu ya kuona umri umeenda sana, sababu ya kuridhisha watu fulani,
sababu kwamba na wao waonekane wameoa au kuolewa, kwasababu alizaa na
muhusika na kadhalika ....kumbuka kama unayemuoa au kuolewa nafsi yako
haijaridhika naye utaishi kwa mateso maisha yako yote.hutaweza kushiriki
tendo la ndoa kwa amani na wala hutaweza kuonyesha mapenzi kwa aina
yeyote ile hata ukijalizimisha utashtukiwa tu.
zingatia swala la imani za kidini; swala hili unaweza kuliona
dogo kabla ya ndoa au ukaliona kubwa lakini ukalifumbia macho kwasababu
umependa lakini kumbuka ndoa haziunganishi watu wawili tu, ndoa
huunganisha familia mbili.utafiti umeonyesha kutoelewana kabisa kwa
familia za imani tofauti zikikutanishwa na ndoa.mfano mkristo kumuoa
muislam. kama unaona familia ya muhusika haijaridhika na iko tayari
kukutenga au kumtenga mwenzako basi achana na hiyo ndoa kwani itakupa
msongo wa mawazo maisha yako yote na siku watoto wakizaliwa ugomvi ndio
utakua mkali zaidi kwani kila familia itataka mtoto afuate imani
yao.kuepusha hili tafuta mwenye imani kama yako au upate baraka za
familia zote kabla ya ndoa na muelewane kuhusu imani za watoto.kumbuka
familia bora ni ile inayosali kwa pamoja.
zingatia swala la ugomvi; kama mtarajiwa wako ameshaanza kukupiga
makofi sasa hivi basi ujue baada ya ndoa itakua mapanga na rungu. mtu
alizeyezoea kupiga hataacha kukupiga kamwe hata akisema atabadilia
usimsikilize kwani muda wa kubadilika ni kabla ya ndoa.kuna watu wengi
sana wameuawa sababu ya vipigo ndani ya ndoa.
zingatia swala la heshima; hii ni muhimu sana hasa kwa wanaume...
wewe ndio unaenda kua baba wa familia hivyo kimsingi kauli ya mwisho
inatakiwa itoke kwako. usioe mwanamke ambaye huwezi kumkemea kufanya
kitu fulani kwani ataitesa nafsi yako mpaka utakapokufa.kama huwezi
kumwambia usifanye hiki akakusikiliza basi huyo hakufai.
zingatia swala la uchumi; uko tayari kuhudumia familia kwa uchumi
wako? utakayefunga nae ndoa ndiye atakaye amua kama mtakua matajiri au
masikini. je unaweza kumiliki mtu ambaye hawezi kujishughulisha kwa
lolote? swala la kusoma au kua na kazi sio muhimu sana kwani kuna mfano
wa watu wengi ambao sio wasomi lakini wana maisha mazuri na kama kasoma
hana kazi huenda atapata siku moja.kama mwenzio haonyeshi dalili ya
kujituma kutafuta pesa, sio mchumi yaani kila siku mnalazimika kula
hotelini na wakati jiko mnalo, ana imani wewe ndio kila kitu basi kimbia
mbali. hali ya dunia kiuchumi ni mbaya sana kuna uwezekano hata ukiugua
muda mrefu au ukifa watoto watakufa na njaa kwani mwenzio anakutegemea
wewe.tafuta muhangaikaji kama wewe au angalau jaribu kumbadilisha kama
akibadilika sawa.
zingatia swala la watoto wa nje; lazima iwekwe wazi watoto
waliozaliwa nje wataishi vipi kama familia.swala hili ni changamoto sana
hasa kwa mwanaume mwenye watoto, mara nyingi wanaume hua hawajali sana
kuishi watoto ambao sio wao lakini wanawake wanaweza kuwapa hata sumu
watoto wa mume.kama huwezi kuvumilia na kuhudumia watoto ambao sio wako
basi achana na hiyo ndoa.uliyezaa nae ni kikwazo kikubwa sana kwa mwenza
wako wa sasa. kaa mbali na huduma zake zote za kifedha au mawasiliano
naye yeyote. anaweza kua na haki ya kuona mtoto, ni vizuri ukampa ratiba
za shule awe anenda kumuona huko lakini walimu wasimruhusu kuondoka
naye.lakini kikubwa ni kwamba kama huna moyo wa chuma basi usijaribu
ndoa hii.
zingatia swala la magonjwa ya kurithi; kama familia zenu zina
magonjwa yanayofanana na ya kurithi mfano albino, siko seli, kifafa,
magonjwa ya akili, na kadhalika basi nendeni mkapime kujua kama kuna
uwezekano wa nyinyi kuzaa watoto wa aina hiyo.japokua baadhi ya vipimo
hapa kwetu havipo.ikithibitika kuna uwezekano wa kuwazaa basi achana na
hiyo ndoa usije kuleta viumbe duniani ambavyo vitateseka sana na wewe
utateseka sana kuwahudumia.
zingatia mahusiano yaliyopita; ni vizuri kujua mahusiano
yaliyopita yaliisha vipi yaani watu waliachana kweli au kuna sababu
ambazo ziko nje ya uwezo wao ziliwafanya waachane lakini bado
wanapendana.mfano umbali kutoka kwa mpenzi wa zamani, yeye aliachwa
lakini bado anampenda, mpenzi kutokua tayari kuoa au kuolewa kwasababu
za kiuchumi au sababu zake binafsi au familia kumkataa.fuatilia kama
kama wana mawasiliano na uhakikishe mapenzi yaliisha na wewe ndio
unayependwa kwa sasa lakini bila hivyo utaendela kusaidiwa na kuna
mifano hai mpaka leo yaani vikao vya harusi vinaendelea lakini mtu bado
anatembea na mtu wake wa zamani.
zingatia tabia za mwenza wako; binadamu tuna tabia mbalimbali na
kila mtu kuna jinsi anazitafsiri tabia hizo kwa upande wake
mwenyewe.kama kuna tabia yeyote ambayo binafsi huipendi kwa mwenza wako
mfano ulevi, umalaya, hapendi, hajui na hataki kupika, kwenda disco,
kuvaa nguo za ajabu, uchafu,kutokwenda kuabudu, matusi, hasira za ajabu,
na ameshindwa kuiacha tabia hiyo kabla ya ndoa basi achana nae na sio
kwamba hataolewa au kuoa lakini waaachie watu wanaoweza kumvumilia.wewe
unaweza kua hupendi kitu hiki ila mwingine haoni kama ni tatizo.
kua mvumilivu;hili ndio swala kubwa ambalo linafanya ndoa za
wazee wetu ziweze kudumu mpaka leo, kama wewe unaona kuna matatizo
yatakuja ukiingia kwenye ndoa au tayari umeshaingia huko na umejikuta
tayari umekabwa silaha ya uvumilivu ndio ambayo unatakiwa uwe nayo sasa
hivi. hata kama ukiingia kwenye ndoa na mtu ambaye hana dosari yeyote
lakini kuna changamoto za hapa na pale lazima zitatokea na inabidi
uzivumilie.
mwisho; mambo niliyotaja hapo juu kuna uwezekano unayaona kwenye
nahusiano yako tayari lakini unashindwa kufanya maamuzi magumu sababu
una mapenzi makubwa juu ya huyo mwanaume au mwanamke. muda kwa kufanya
maamuzi ni sasa kama huamini waulize walioingia tayari na sasa wanajuta.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni