Kocha Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte amesisitiza kuwa kiungo, Cesc
Fabregas ni mtu muhimu na bado yumo kwenye mipango yake msimu huu, licha
ya kutomtumia katika mechi nne za mwanzo za Ligi Kuu England mpaka
sasa.
Fununu zilizopo juu ya majaaliwa ya Mhispania huyo ni kwamba huenda
akapisha njia kikosini hapo kutokana na kocha huyo kuwatumia zaidi Oscar
sambamba na Nemanja Matic na N'Golo Kante aliyetua msimu huu.
Hata hivyo alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumuuza Fabregas kwenye
dirisha dogo la usajili, Januari, Conte alijibu: "Hapana, hapana,
hapana. Cesc bado yumo kwenye mipango yangu na mimipango ya Chelsea pia.
Sote tunajua Cesc ni mchezaji hatari. Katika kila mazoezi, namuona ni
mtu mwenye ari kubwa. Kama akiendelea namna hii, nitakuwa na wakati
mgumu kuchagua kiungo wa kumtumia.
"Hiki ndicho ninachokitaka kwa mchezaji, niwe na hofu ya nani nimchague
kucheza. Cesc ni mchezaji mkubwa, kila mmoja anamjua. Na sasa naanza
kumuelewa kama mwanaume wa kazi.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni