Kurasa

Alhamisi, 15 Septemba 2016

Elimu kwa wakimbizi haipewi kipaumbele-Ripoti ya UNHCR

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mustakhbali wa wakimbizi na wahamiaji ukikaribia kufanyika, imeelezwa kuwa zaidi ya watoto Milioni Moja na Nusu ambao ni wakimbizi hawaendi shuleni.

msichana ambaye ni mkimbizi tangu utotoni.. anakumbuka wosia wa mama yake, kuhusu umuhimu wa kwenda shule…

Msichana huyu na wengine wengi ni miongoni mwa takwimu zilizotolewa leo na UNHCR zikisema kuwa fursa ya elimu kwa watoto wakimbizi ni finyu au haipo kabisa.

Shirika linasema ni dhahiri kuwa elimu kwa watoto wakimbizi imetelekezwa, elimu ambayo ni fursa pekee ya kubadili maisha ya maelfu ya watoto waliosambaratishwa na vita..

Ripoti hiyo inasema wakimbizi wanakosa fursa ya elimu mara tano zaidi ya wastani wa elimu ya kimataifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni