Mgombea urais wa
chama cha Democratic nchini Marekani Hillary Clinton atarejelea kampeni
zake mnamo Alhamisi, msemaji wake amesema.
Mwanasiasa huyo alikuwa amepumzika kwa siku kadha ili kupata nafuu baada ya kuugua kichomi.Bi Clinton alizidiwa na nusura azirai alipokuwa anahudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 15 tangu kutekelezwa kwa shambulio la kigaidi la 9/11 ambapo watu karibu 3,000 waliuawa.
Aligunduliwa kuwa anaugua kichomi, ugonjwa wa mapafu ambao pia hujulikana kama nimonia, siku ya Ijumaa.
Kumezuka mjadala mkali kuhusu afya yake Marekani, na muda ambao alichukua kupata nafuu, huku uchaguzi mkuu ukiendelea kukaribia.
chanzo: bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni