Kurasa

Jumamosi, 8 Oktoba 2016

Trump akabiliwa na kashfa nyingine

Dolnald Trump

Viongozi wandamizi wa chama cha Republican nchini Marekani wamelaani matamshi yaliyotolewa na mgombea urais wa nchi hiyo kupitia chama hicho Dolnald Trump aliyoyatoa mwaka 2005 yakimdhalilisha mwanamke.
Katika mkanda huo wa video uliotolewa na gazeti la Washington Post, Trump anasikika akimwambia mtangazaji wa kipindi kuwa unaweza kufanya jambo lolote kwa mwanamke ukiwa nyota.
Trump ameomba radhi katika taarifa aliyoitoa kupitia video mapema leo,lakini wakati huo huo Spika wa Bunge la Congress ambaye alikuwa afanye kampeni na Trump baadae leo amejitoa na hatahudhuria mkutano huo ambao ungefanyika katika jimbo la Spika Ryan huko huko Wisconsin.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni