Kurasa

Jumapili, 25 Septemba 2016



WAWAKILISHI WA CCM WATAKA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR IWE YA CCM PEKEE ISISHIRIKISHE VYAMA VYENGINE VYA SIASA.
BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM, wameibua hoja nzito wakitaka Sheria ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ifanyiwe mabadiliko na kuwaondoa wajumbe wa tume wanaotokana na vyama vya siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Hoja hiyo imesababisha marekebisho ya 11 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yaliyokuwa yawasilishwe jana katika mkutano wa tatu waBaraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) kukwama na kutoa muda wa kujadili hoja zilizojitokeza.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao cha Wawakilishi wa CCM waliokutana kujadili marekebisho hayo kabla ya kuwasilishwa Barazani wanataka kifungu cha 119 (1) cha Katiba ya Zanzibar kinachozungumzia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kifanyiwe marekebisho, Rais aweze kufanya uteuzi wa wajumbe wa Tume bila kushauriana na kiongozi wa upinzani Barazani au vyama vya siasa.
Chanzo:Hababi Cuf

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni