Takriban wanajeshi
saba nchini Niger wameuawa katika kipindi cha juma moja lililopita
kufuatia makabiliano kati yao na wapiganaji wa Boko Haram ,jeshi la
taifa hilo limesema.
Wanajeshi wa Niger wakisaidiana na wenzao
kutoka Chad walivamia kambi ya wapiganaji hao na kuwaua 30 na kuwakamata
wawili ,msemaji wa jeshi amesema.Mashambulizi hayo mawili yalifanyika kusini mashariki mwa jimbo la Diffa karibu na mpaka na Nigeria,taarifa ilisema.
Wanajeshi watano waliuawa katika uvamizi mwengine siku ya Jumatatu asubuhi na wengine wawili wakauawa baada ya gari lao la kupiga doria kukanyaga bomu la ardhini,taarifa hiyo imeongeza.
Mashambulio ya miaka saba yanayotekelezwa na kundi la Boko Haram yamesababisha vifo vya maelfu ya watu nchini Nigeria ,ambapo ndio ngome kuu ya wapiganaji hao,pamoja na maeneo jirani ya Niger,Chad na Cameroon.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni