Maafisa wa umoja wa mataifa wameonyesha hasira juu ya kushindwa kwao
kusambaza misaada ya kibanadamu huko Syria, licha ya usitishwaji wa
mapigano kuanza tangu siku ya jumatatu.
Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa nchini Syria, Staffan de Mistura
amesema kuwa serikali ya nchi hiyo haijatoa kibali cha kuruhusu
usambazaji wa misaada kama walivyoahidi, huku mshauri wa masuala ya
kibinadamu Jan Egeland anawashutumu waasi huko Aleppo kwa kucheza mchezo
wa kisiasa.
Washirika wakuu wa Rais Assad, Urusi wamesema kuwa vikosi vya serikali
vimeondoka katika barabara kuu ya kuelekea mji wa kaskazini mwa Aleppo,
hii ikimaanisha kuwa msafara wa misaada wa umoja wa mataifa unaweza
kufika katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi siku ya leo.
Lakini Marekani inasema kuwa haina uhakika kama kuondoka huko kumeanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni