Katibu mkuu wa
umoja wa mataifa Ban Ki-moon amemkosoa vikali waziri mkuu wa Israel
Benjamin
Netanyahu kwa pendekezo lake kwa wale wanaopinga upanuzi wa
makazi ya Israel kuwa wao ni wafuasi wa kikabila.
Ban Ki-moon amesema kuwa maoni ya Netanyahu hayakubaliki na ni ya kichochezi.
Ban Ki-moon ambae anaondoka madarakani mwisho wa mwaka huu amewakumbusha Israel kuwa upanuzi huo wa makazi sio halali chini ya sheria ya kimataifa, na kwa lugha ya ukali Ban Ki-moon alisema Urusi lazima imalize ukandamizaji na uvamizi wa maeneo ya Palestina.
Chanzo: bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni