
Maafisa wa Serikali ya Korea Kusini
wamefichua kuwa serikali ina mipango ya kuharibu kabisa mji mkuu wa
Korea kaskazini, iwapo ishara yo yote itaonekana kuwa kuna mipango ya
kushambuliwa kwa nukilia.
Shirika la Habari la Yonhap lililo na uhusiano mkubwa na Korea Kusini linasema kwamba wabunge nchini humo wamepewa mpango huo.Mpango huo unanuia kuharibu kabisha makombora yote yaliyo na zana hatari kukiwemo nukilia.
Ufichuzi huu unatokea siku mbili baada ya Korea Kaskazini kulipua angani jaribio kubwa zaidi la kinukilia, ambalo limetoa dhana kuwa Korea Kaskazini imepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa zana za kinukilia.
Chanzo: BBCswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni