
MUANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA....
“Meneja hizo pesa nitoe za benki au zako binafsi?”
“Toa za benki mtu akikuuliza, muambia aje kwangu”
Bwana Turma akiwa anasubiria zoezi la kufungiliwa akauti, gafla milio mingi ya risasi ikaanza kusikika ikitokea nje na kuanza kuwachanganya bwana Turma na muhasibu wake
ENDELEA......
Kitendo cha wasichana, makatili kuiingilia bank ya CNB, na kuwazalilisha wananchi walio kuwemo ndani ya benki kwa kuwatoa nje uchi kinazidi kuiumiza serrikali.Isitoshe inamuwia ugumu Bwana Turma, na akashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano maalumu kwani gari lake la thamani, limehusika katika matumizi ya uvamizi wa Benki.
Dickson anatoa nje ya kibanda chake, huku akiwa na wasiwasi mwingi akiwatazama askari wawili wanaokuja kwenye kibanda chake
“Habari yako kaka?”
Askari mmoja alimsalimia Dickson
“Salama tuu mambo vipi?”
ILIPOISHIA....
“Meneja hizo pesa nitoe za benki au zako binafsi?”
“Toa za benki mtu akikuuliza, muambia aje kwangu”
Bwana Turma akiwa anasubiria zoezi la kufungiliwa akauti, gafla milio mingi ya risasi ikaanza kusikika ikitokea nje na kuanza kuwachanganya bwana Turma na muhasibu wake
ENDELEA......
Kitendo cha wasichana, makatili kuiingilia bank ya CNB, na kuwazalilisha wananchi walio kuwemo ndani ya benki kwa kuwatoa nje uchi kinazidi kuiumiza serrikali.Isitoshe inamuwia ugumu Bwana Turma, na akashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano maalumu kwani gari lake la thamani, limehusika katika matumizi ya uvamizi wa Benki.
Dickson anatoa nje ya kibanda chake, huku akiwa na wasiwasi mwingi akiwatazama askari wawili wanaokuja kwenye kibanda chake
“Habari yako kaka?”
Askari mmoja alimsalimia Dickson
“Salama tuu mambo vipi?”
Dickson alizungumza kwa kujikaza tuu, kuuficha wasiwasi wake kwa maana msichana ambaye ni Rahab aliye muacha ndani anaonekana hana masihara kabisa katika matumizi ya silaha
“Hukuona, msichana aliye vaa akipita katika maeneo haya?”
“Ahaaa kusema kweli, sijamuona kwa maana hizi bunduki kwa jinsi zilivyokuwa zikinguruma huko nje sikudhubutu hata kuitoa miguu yangu”
Askari wakamtzama kwa umakini Dickson, ambaye anazungumza kwa kubabaika
“ Basi tunakuomba ufunge duka lako”
“Sawa”
Askari wakaanza kuondoka na kurudi katika eneo walipo wazao, Dickson akarudi ndani huku jasho jingi lkimwagika mithili ya maji.
“Waameniambia nifunge”
Dickson alimsemesha Rahab ambaye kichwa chake amekiinamisha kwenye ukuta huku sura yake ikitazama juu.
“Dada, dada.Wamesema nifunge duka langu”
Rahab hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya, huku akimtazama Dickson jinsi sura yake inavyo mwaga jasho jingi
“Powa”
Rahab alijibu kwa kifupi, na kuzidi kumchanganya Dickson
“U...takaa humu ndani?”
“Ndio wewe funga”
“Mmmm”
Dickson akabaki akiwa anashangaa shangaa, Rahab akainyanyua bastola yake na kumuwekea Dickson ya kichwa, mwili mzima wa Dickson ukawa kama umepigwa na shoti ya umeme, taratibu suruali yake ikaanza kutengeneza mchoro sehemua ya zipu, kwani woga umemfanya hadi ameshindwa kuzuia haja ndogo
“Huwa sipendi, nizungumze mara mbili mbili.Potea”
Rahab alizungumza huku sura yake akiwa ameikunja, na anaonekana kuwa na hasira kali.Kwa hahara Dickson akatoka nje ya kibanda chake, na kuaanza kufunga geti la kaduka kake hata baiskeli anazo zitengeneza hakukumbuka kuziingiza ndani.Kwa kuchanganyikiwa akajikuta akitembea asijue ni wapi anaelekea
Wote wanne wakiwa na bunduki zao mikononi, wakawa wanaitazama njia ambayo ni yakuingilia kwenye eneo lao la handaki.
“Tutawanyike wawili wawili”
Fetty alizungumza huku akiikoki bunduki yake, Anna akamfwata Fetty huku Halima na Agnes wakiwa wamesimama sehemu moja.Wakatazamana kwa muda pasipo mtu yoyote kuzungumza neno , kisha wakaanza kukimbia mtuni, wakiwa wameganawana kila watu wawili sehemu yao.Fetty na Anna walielekea magharibi mwa msitu wao, huku Agnes na Halima wakielekea Mashariki mwa msitu wao.
Askari wakiongozwa na mbwa wao, walio fundishwa mafunzo maalumu ya kunusa kila sehemu ambayo amepita mtu ambaye askari wanamuhitaji, ndivyo walizidi kuendelea kuingia msituni wakiwa na bunduki zao.Huku kila mmoja akiwa na hasira kali juu, ya maauaji yaliyo tokea siku chache zilizo pita juu ya wezao walio uwawa kwenye kituo cha gesi kwa mlipuko mkali.Amri mmoja iliyo tolewa na mkuu wa jeshi la polisi Bwana Gudluck Nyangoi ni kwamba wahakikishe wanawatia nguvuni ili wahukumiwe kifungo kikali kitakacho ishangaza dunia
Askari wakiongozwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Ngurumo, wanaendelea kuuzingira msitu huku wakiwa na imani ya kufanikiwa na abushi yao wanayo kwenda kuifanya kwenye msitu unao sadikika ndipo walipo ingia majambazi kipindi wakitokea kufanya tukioa benki, na maelezo haya yalitolewa na msamaria mwema ambaye, gari lao lilisimamisha kipindi askari wa usalama barabarani walipokuwa wakifanya uchunguzi kwa kila gari ambalo lilikuwa likikatiza katika barabara kuu ya kuelekea mikoa ya Tanga na Arusha
Wakiwa katikati ya msitu, mbwa wao wakaanza kubweka kwa sauti ya juu, na kuzidi kuwastua askari na kuamini kuna jamba ambalo lipo kwenye eneo ambalo wamefika.
“Waachie mbwa”
ACP Ngurumo aliwaamrisha askari sita walio washika mbwa wao, Mbwa wakaanza kuelekea katika maeneo walipo Fetty na Anna, ambao bunduki zao wameziweka tayari kwa kila kitu. Kwa kutumia bunduki zao zenye lensi ya kuvuta mtu kwa ukaribu sana, Fetty akawashuhudia mbwa wakiwakaribia katika eneo walilo jificha huku kwa nyuma kukiwa na kundi la askari wapatao sita, wakiwa na bunduki mikononi mwao.Anna akaishika bunduki yake, kabla hajafyatu risasi Fetty akamzuia
“Ngoja nikuonyeshe mchezo, wasikumalizie risasi zako”
Fetty alizungumza huku akikichomo kisu chake, kikali na kirefu sana mfukoni,
“Anna nilinde”
“Powa”
Fetty akaanza kutambaa kwa haraka kuuelekea mbwa wanapo tokea na na askari wao, akajibanza kwenye mti mkubwa ambao ndio njia ambayo mbwa na askari ndio wanatokea, Macho ya Anna yakawa na kazi ya kuwatazama askari wanao kimbia kwa kasi wakiwa nyuma ya mbwa wao, Fetty akachomoa kisu kingine kinacho fanana na kisu alicho kishika mkono wake wa kulia, Akashusha pumzi kidogo kisha akachungulia kidogo sehemu wanapo tokea mbwa na kuwaona wakiwa wamebakisha hatua chache kutoa sehemu alipo jificha
“It’s My time now”(ni wakati wangu sasa)
Fetty alizungumza huku akishusha pumzi nyingi, kwa haraka akachuchumaa chini, kitendo cha mbwa wa kwanza kujitokeza sura yake usawa wa Fetty, ikawa ndio muda wa mbwa huyo mwenye kasi kupita wezake, kukumbana na kisu cha koo na kumfanya kutoa ukelele mmoja tuu, mithili ya panya aliye banwa na kitu kizito na kutulia kimya.Akaskari wakasimama baada ya kuona mbwa wa kwanza akiwa amepotea gafla, kasi ya mbwa wengine watano ikaanza kupungua na kuwa ya kusita sita baada ya kumuona mwenzao akiwa ametupwa katika njia waliyo kusudia kupita, huku akiwatokwa na damu nyingi.
Askari kwa kuchanganyikiwa wakaanza kufyatua risasi pasipo kuwa na mpangilio maalumu, kwani hawakujua ni wapi alipo jifich mtu aliye sababisha kifo cha mbwa huyo, ambaye anaaminika sana kupita mbwa wote.Fetty akaachia tabasamu pana, huku akiwa amejibanza kwenye mti aliopo wenye unene kiasi, unao msaidia kutokuweza kuonekana, wala risasi kumfikia alipo.
“Nyinyi kuna kitu gani kinacho enelea huko.OVER”
Sauti ya Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) bwana Ngorumo ilisikika kupitia simu ya upepo, hii ni baada ya kusikia milio ya risasi nyingi zikimiminika.
“Wapo, huku mkuu, Over”
Askari mmoja alizuingumza huku akiendelea kufyatua fyatua risasi ovyo
“Tunakuja, Over”
Macho ya Anna yakakutanana na macho ya Fetty ambaye, akaendelea kumkonyeza asifanye kitu chochote cha kijinga.Anna akazidi kupatwa na wasiwasi kwani akujua ni kitu gani kinachompa ujasiri Fetty kuendelea kung’ang’ania nyuma ya mti alio uegemea
Fetty akatupa visu vyake chini na kuchomoa bastola mbili kwenye viatu vyake, ambazo zimejaa risasi za kutosha, kwa ishara ya mmdomo pasipo kuzungumza kwa sautia, Anna akamtaarifu Fetty kwamba askari wameongezeka katika eneo walilopo.Askari walioongezeka kwenye eneo walipo wezao, bila hata ya kuuliza ni wapi walipo majambazi, wao wakaanza kufyatua risasi zao wakishambulia kile eneo
“Zima motoo”
ACP Ngurumo alizungumza kwa sauti ya juu, baada ya kuona risasi zao zikiendelea kumiminika pasipo kuwa na mafanikio yoyote ya kuua majambazi
“AK47 tangulia mbele”
Aliwaamrisha askari wenyebunduki aina ya AK47 kupita mbele, huku wengine wanye bunduki aina ya SMG wakiwa wamebaki nyuma ya wezao huku wamelala chini.Askari wapatao nane wenye bunduki aina za AK47, wakaanza kutembea kwa kunyata wakielekea ulipo mti ambao pembeni kuna mbwa wao aliye lala chini, tayari akiwa amekata roho.
Kwa kutumia ishara ya vidole Fetty akaanza kunyanyua kimoja, kikafwata cha pili, hadi cha tatu anakinyanyua, Anna akaanza kufyatua risasi mfululizo kwa askari wote nane wenye bunduki aina ya AK47, na hakuna hata mmoja aliye baki akiwa amesimama kwani, risasi zote alizo zifyatua kwa kutumi bunduki yake aina ya ‘M8AI’, zilitua vichwani mwa askari hao.
Askari walio lala chini wakaanza kuchanganyikiwa kwa shambulizi walilo fanyiwa wezao, wakaanza kufyatua risasi kuelekea sehemu yenye jiwe kubwa alipo lala Anna, na kusahau kuuangalia mti ambao askari nane walio uwawa walikuwa wakinyata,Fetty kwa kutumia bastola zake mbili, moja ikiwa aina ya ‘COLT 1911’ huku nyingine aina ya ‘DESERT EAGLE’ akaanza kuwashambulia askari kwa nyuma, walio kuwa wameelekea upande alipo jificha Anna.Kila mmoja akaanza kuchanganyikiwa kwani kila alipojaribu kufyatua risasi walipo majambazi ndivyo alivyo jikuta akianguka chini na kupoteza maisha yake hapo hapo.
Hadi shambulizi linazima, akabaki Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Ngurumo akiwa amelala chini akiwashuhudia maiti za askari wake wakiwa wamelala chini, wakivunjwa na damu nyingi mwili mzima.Fetty akapiga hatua za umakini hadi sehemu alipo lalaa ACP Ngurumo, na kumuwekea risasi ya kichwa
“Fetty”
Anna aliita kwa sauti ya juu, na kumfanya Fetty kutazama sehemu alipo Anna na kumuona akiwa amesimama huku akiwa anavujwa na damu za paja lake la kushoto, ikiashiria katika risasi zote zilizo fyatuliwa na askari hao kuna iliyo mpiga kwenye mguu wake
Agnes na Halima waliendelea kuzisikia kelele za risasi nyingi, ila hawakudhubutu kunyanyuka sehemu walipo kwenda kwani hawakujua ni wapi risasi hizo zinapo tokea.Kila wanapojaribu kutazama sehemu zote za msitu wanaona ukimya mwingi baada ya risasi nyingi zilizo fyatuliwa zaidi ya nusu saa
“Mbona mapigo yangu ya moyo yanakwenda kasi”
Halima alizungumza huku akinyanyua kichwa chake akitazama mbele yao, pasipo kuona kitu chochote
”Acha uoga chost” Agnes alijibu
“Sio woga, ila mapigo yanakwenda mbio, haijawahi kutokea siku hata moja”
“Hembu ngoj.......”
“WEKENI SALAHA ZETU CHINI, WANAHARAMU NYINYI”
Kabla hata Agnes hajamalizia sentesi yake sauti ya ukali ikawamrisha nyuma yao, wakageuka kwa haraka na kukutana na kundi la askari wapatao kumi wenye bunduki mikononi mwao, huku bunduki zao zote zikwa zimeelekea upande wao, na sura za askari hawa zimejaa mikunjano inayo ashiria hasira kali walizo nazo....
Endelea na sehemu ya 14 kupitia ubuyublog.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni