Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul makonda
amezindua Muonekano mpya wa waendesha Bodaboda na bajaji katika Mkoa wa
dsm ambapo hivi sasa watakuwa na Mavazi maalum ya kuwatambua,Vituo
sambamba na namba maalum katika mavazi yao ili kuboresha huduma hiyo na
kuwatambua wahalifu wanatumia bodaboda kutekeleza uhalifu wao.
Aidha Makonda amezindua chama cha madereva na wamiliki wa pikipiki na
bajaji katika mkoa wa dsm chenye wanachama 45,000/= ambapo amewataka
kuheshimu sheria huku serikali,jeshi la Polisi pamoja na Sumatra ikiweka
mpango madhubuti wa kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia
sheria na taratibu zilizowekwa.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya leaders
kinondoni,Makonda amesema kuanzishwa mfumo huo mpya ambapo kila wilaya
madereva hao watambulika kwa mavazi yao,namba kutasaidia kupunguza
changamoto za uhalifu,lakini kuwezeshwa kupitia chama chao.
Chanzo:muungwana blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni