Dar Es Salaam.Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu kifungo cha
mpaka 30 jela, Rashid Mohamed (32)baada ya kupatikana na hatia na
kubaka mtoto wa miaka 13.
Mohamed ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Chanika amehukumiwa
kutumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kuridhika na ushahidi wa
mashahidi sita waliotoa dhidi yake.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Juma
Hassani amesema mahakama yake imemtia hatiani kama alivyoshtakiwa.
"Nimejiridhisha na ushaidi uliotolewa mahakamani hapa pasina kuacha
shaka, hivyo Mohamed atatumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe
fundisho kwa vijana wenye tabia chafu kama yako" alisema Hakimu Hassan
Awali kabla ya hukumu hiyo kutolewa Wakili wa Serikali, Grace Mwanga
aliiambia mahakma hiyo kuwa hakukuwa na kumbukumbu zozote za mshtaka ya
nyuma dhidi ya mshatakiwa na hivyo kuiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu
kama sheria inavyoeleza.
"Kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji dhidi ya watoto,
naiomba mahakama yako itoe adhabu kali dhidi ya mshatakiwa huyu ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizi " alidai Mwanga.
Katika hati ya mashtaka, Mohamed alitenda kosa hilo, Desemba 15, mwaka jana eneo la Chanika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni