Kutokana kugundulika kwa matumizi ya nishati ya gesi asilia nchini mpaka sasa serikali imekoa zaidi ya shillingi trillion 14 mwaka 2014-2015 ikiwemo kuwepo kwa umeme wa uhakika hapa nchini.
Akitoa mada wakati wa swmina kwa waandishi wa habari mkoani Morogoro juu ya mafanikio ya kupatikana kwa gas tanzania mhandisi wa shirika la maendeleo ya petrol Tanzania TPDC Felix
Nanguka amesema shughulli nyingi za kiuchumi zimehamia katika matumizi ya gesi na kupunguza gharama kubwa za matumizi ya mafuta mazito hali iliyopelekea kuzalishwa kwa umeme wa gesi kuenea katika viwanda vikubwa na vidogo huku akidai tafiti zanaonyesha kuongezeka kwa pato la taifa baada ya kukamilika kwa mitambo yote ya gasi.
Aidha afisa uhusiano wa shirika la maendeleo ya petrol tanzani TPDC Francis Lupokela amesema katika shughuli za ujenzi na ulinzi wa miundombinu ya kusafirishia gesi asilia hapa nchini shirika la limewanufaisha wananchi katika upatikanaji wa ajira nae mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari morogoro Nicksoni Mkilanya amesema mafunzo hayo yatawasaisdia waandishi kuhamasisha na kuandika habari za mafuta na gesi kwa ueledi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni