
Akina dada wa Manchester City wameshinda kombea la ligi kuu ya wanawake kwa mara ya kwanza baada ya kuwashinda akina dada wa Chelsea kwa mabao 2-0 na kutangazwa mabingwa.
Manchester City ambanao hawajashindwa walihitaji ushindi ili kuweza kuongoza.
Nahodha wa Chelsea Katie Chapman aliifunga klabu yake mwenyewe baada ya kona iliyopigwa na Toni Duggan dakika 12 kabla ya mapumziko.
Duggan alifunga bao la pili kwa njia ya penalti baada ya Lucy Bronze kuchezewa vibaya.
Ushindi wa City uliwaweka kileleni kwa pointi 10 mbele ya Chelsea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni