Timu hizo zinatarajiwa kukutana Oktoba Mosi, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mahadhi alisema kutokana na ubora wa kikosi cha Yanga kwa sasa, haoni kama kuna timu itawazuia huku akisisitiza kwamba amejipanga kufanya vizuri siku hiyo.
“Kiukweli kwa sasa ndani ya Tanzania, Yanga ndiyo timu bora kutokana na kikosi ilichonacho pamoja na mafanikio ya ushiriki wa michuano mikubwa na ni ajabu kukaa kuihofia timu kama Simba kwa sababu tayari tumeshacheza na timu kubwa na ngumu kuliko hiyo,” alisema Mahadhi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni