Kurasa

Alhamisi, 22 Septemba 2016

Harmonize: Nilishawahi Kuwa Dereva Bodaboda

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Matatizo’ amefunguka na kusema kuwa katika harakati zake za kutafuta maisha alishawahi kuwa dereva wa bodaboda. 
Harmonize amesema aliifanya kazi hiyo katika kuhakikisha anaendesha maisha yake kabla ya yeye kutoboa kwenye mambo ya muziki. 
Akiongea kupitia kipindi cha ‘Ngazi kwa Ngazi’ kinachorushwa na EATV Harmonize alisema kuwa anakumbuka mwaka 2011 alikuwa akifanya kazi hiyo ya kuendesha pikipiki na kubeba abiria ndiyo maana ana uzoefu mzuri wa kuendesha Pikipiki kutokana na kazi yake hiyo aliyoifanya kwa muda fulani. 
“Unajua mimi nilishawahi kuwa dereva bodaboda nakumbuka ilikuwa mwaka 2011 nilikuwa nafanya kazi ya kubeba watu na Pikipiki hivyo nina uzoefu mzuri tu wa kuendesha Pikipiki, nilikuwa nabeba abiria hapa na pale najipatia riziki ndiyo maana hata katika video yangu ya ‘Bado’ niliona niendesha tu ile pikipiki 

kwa kuwa nilikuwa na uzoefu wa kuendesha pikipiki, ” alisema Harmonize

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni