Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli aliyevuma kitambo, amefunguka na kusema kuwa kitendo cha msanii Diamond Platnum kurudia moja ya kazi yake anajihisi kuzaliwa upya.
Saida Karoli ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Mapenzi kizunguzungu’, Kaisiki, Maria Salome na nyingine kibao na alifanikiwa kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa nyimbo hizo na kujipatia umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Saida Karoli amesikika kwenye moja ya clip ambayo ameiposti Diamond Platnumz kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mwanzoni waandishi wa habari walisha msahau walikuwa hawamtafuti tena, lakini hata baadhi ya watu pamoja na ndugu zake walikuwa wakiambiwa kuwa amekufa lakini baada ya kazi ya Diamond Platnumz kutoka imerejesha watu kwenye himaya yake kwani wameanza kumtafuta na kumpigia simu sana.
“Mimi nimejisikia vizuri maana hii kazi tunayofanya ni kwa ajili ya mashabiki, mashabiki ndiyo wadau wetu wanaotufanya sisi tuwe juu kwa hiyo si kazi ya kwangu mimi peke yangu, ila mimi kama mimi nimejisikia vizuri kusikiliza kwa sababu hata vyombo vya habari vilinisahau leo hii vinanitafuta, haya ndugu zangu baadhi na wengine wanajua hata siko duniani wanajua nilishakufa lakini leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta kweli nimefunguka najihisi kuzaliwa upya” alisikika Saida Karoli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni