Mkurungezi mtendaji mkuu wa Microsoft Satya Nadella
Kundi hilo limesema limepokea mamia ya malalamishi kuhusiana na uboreshaji wa programu hiyo .
Watumiaji wa programu hiyo wanalazimika kulipia komputa zao ili zirekebishwa kutokana na faili kupotea.
Hatahivyo Microsoft ilitetea programu hiyo ya Windows 10 na kusisitiza kuwa imekuwa ikitoa usaidizi kupitia mtandaoni na vilevile kwa simu.
Imeongezea kwamba itawasaidia watu kupata programu yenye manufaa na yenye usalama dhabiti, kulingana na msemaji wa kampuni hiyo.
Programu ya Windows 10 hutumika kwa simu aina ya smartphone
Pia kumekuwa na malalamiko kuhusiana na huduma mbaya kwa wateja wake,pale wanapohitaji msaada kutoka kwa kampuni hiyo.
Programu hiyo ya windows 10 ilizinduliwa mwezi Julai mwaka 2015, na hutumika katika tarakilishi,simu aina ya smartphone, na vifaa vya kusikilizia sauti vya HoloLens.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni