
Baada ya mashabiki wa soka ulimwenguni
kusubiria kwa hamu mchezo wa derby wa Man United dhidi ya Man City
katika uwanja wa Old Trafford huku kivutio kikubwa kikiwa ni kocha
mwenye maneno mengi Jose Mourinho akichuana na kocha mwenye falsafa za
kufundisha soka la kucheza mpira na pasi Pep Guardiola Septemba 10,
ilikuwa mwisho wa ubishi.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa 17 kwa
Jose Mourinho na Pep Guardiola kukutana wakiwa wanafundisha vilabu
tofauti tofauti, mchezo umemalizika kwa Man United iliyochini ya Jose
Mourinho kufungwa goli 2-1 wakiwa katika dimba lao la Old Trafford, huku
magoli ya Man City yakifungwa na Kelvin De Bruyne dakika ya 15 na
Kelechi Iheanacho kufunga goli la pili dakika 6 kabla ya Ibrahimovic
kufunga goli kufutia machozi kwa Man United dakika ya 42
Hii ni mara ya 172 kwa vilabu vya Man United na Man City kukutana, licha ya kupoteza mchezo wa leo Man United anaongoza kuifunga Man City mara 71, sare 51 na Man City wameifunga Man United mara 50, kwa upande wa Mourinho leo anakuwa kafungwa na Guardiola mara ya 8 katika mechi 17 walizokutana na kutoka sare mechi 6 na yeye kawahi kumfunga Gurdiola mara 3 pekee.
kutazama magoli angalia linki hii hpa >https://youtu.be/NnudyOyoFWk
chanzo millardayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni