Kurasa

Jumatano, 14 Septemba 2016

CHAMA KIPYA KINAKUJA?


Mhe. Mtatiro, kuna gazeti nimesoma linaeleza kuwa kuna chama kipya kitasajiliwa hivi karibuni: kitaitwa The Civic Democratic Party, CDP. Mwenyekiti wake atakuwa Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti) na Dk. Wilbroad Slaa (Katibu Mkuu). Je ukweli ni upi? Na je hamuoni kuwa combination yao itadhoofisha nguvu za vyama vyenu?
Chidide Muhano,
Mwanza.
MAJIBU:
#Ndugu yangu Chidide. Shida ya watanzania kwa sasa siyo vyama, msajili anavyo 22 and YET ni vyama vinne tu ndivyo vimejaribu kuwa na angalau mbunge mmoja na kuendelea, dhidi ya CCM.
#Ukiachilia mbali UKADA wangu katika CUF na kwa hiyo naweza kutokuwa NEUTRAL, lakini uchambuzi wa kawaida wa masuala ya kisiasa unanifanya nikuhitimishie kuwa kwa siasa za Tanzania zilipofikia, vyama vitakavyoanzishwa hivi sasa vitahitaji miongo miwili hadi mitatu ili kujijenga na kushindana.
#Kwa bahati mbaya, vyama tawala barani Afrika huhusika katika kulea migawanyiko kwenye vyama vilivyopo ili kikundi kitakajiondoa nacho kisajiliwe kama chama. Jambo la msingi ni kuwa, vyama vinavyoanzishwa ili kukata kiu na kutekeleza ajenda za vyama tawala, havikuwahi kudumu. Kwa sababu uanzishwaji wake peke yake ni UDHAIFU, kwa hiyo ukuaji wake pia huwa dhaifu na mwishoni hufa.
#Kwa sababu hiyo, sijawahi kuwa na hofu na vyama vipya, hususani vile vinavyoanzishwa kwa msukumo wa dola, hivi hujifia na haviwezi kufika popote.
#Kuhusu hayo ya Prof. Lipumba na Dk. Slaa, sielewi chochote, waulize wao kupitia mawasiliano yao.
Mtatiro J

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni