Kurasa

Ijumaa, 16 Septemba 2016

Arusha ;TRA Kuvibana Vituo vya Mafuta

 
Arusha. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewataka wamiliki wa vituo vya mafuta mkoani hapa kutumia mashine za kielekroniki kutoa risiti (EFD) la sivyo  watavifunga.

Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha, Robert Manyama alitoa kauli hiyo jana kwenye kikao na wamiliki wa vituo hivyo.

Manyama alisema ni marufuku vituo vya mafuta kutumia risiti za mikono na kama mashine za EFD zikiwa mbovu, mmiliki anapaswa kuwasiliana na wakala aliyemuuzia mashine na kutoa taarifa TRA.

Meneja Msaidizi  wa TRA Kitengo cha Madeni, Irene Hance alisema matumizi ya mashine za EFD yatawasaidia wamiliki wa vituo hivyo kutunza kumbukumbu zao na kulipa kodi stahiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni