Kurasa

Ijumaa, 16 Septemba 2016

kauli ya Prof. Ndulu Kurudisha Imani kwa Watanzania

Profesa Benno Ndulu.

SIKU moja baada ya Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu kueleza kuwa hali ya uchumi iko imara, wasomi na wachumi wameibuka wakisema amerudisha imani iliyopotea na kwamba wananchi wawe wavumilivu.

Kwa wiki moja sasa kumekuwa na mjadala kuhusu hali ya uchumi, huku wachambuzi na wanasiasa wakielezea hali ya maisha ilivyo ngumu kutokana na fedha kupotea mikononi mwa watu.

Miongoni mwa wanasiasa waliochambua hali ya uchumi ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ambaye alisema kuwa kumekuwapo na mdororo wa uchumi ikilinganishwa na mwaka jana.

Pia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, akiwa bungeni wiki iliyopita, alielezea namna deni la taifa lilivyopanda huku hali ya maisha ikiendelea kuwa ngumu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni