Kurasa

Jumatano, 16 Novemba 2016

Nigeria yakumbwa na njaa kali

Nigeria
Mtoto akipatiwa huduma ya dharula

Umoja wa Mataifa umetoa tamko kwamba wanaijeria wapatao nilioni kumi na nne wanahitaji misaada ya kibinaadamu upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo, mahali ambako maelfu kwa mamia ya watoto wako kwenye hatari kubwa ya kifo kutokana na njaa kali na kwamba watoto laki nne wanahitaji msaada wa dharula.


Inaelezwa kuwa mkoa uliokumbwa na baa hilo la njaa awali ilikuwa ngome ya zamani ya kundi la dola ya kiislamu Kiislam, Boko Haram.Jimbo hilo lilikuwa katika hali tete kiasi cha kutokufikiwa na misaada ya kibinaadamu kwa miaka kadhaa sasa ambapo kwa sasa ndiyo limebainika kuwa na hali mbaya ya chakula na njaa kali ikiwemo majimbo ya Borno,Yobe na Adamawa.

Shirika la kuwasaidia watoto la , Unicef, limesema kwamba inakadiwa kuwa watoto wapatao elfu sabini na watano wako katika hatari ya kufa.

Mapema , shirika la misaada ya kitabibu la madaktari wasio kuwa na mipaka wamegundua idadi kubwa zaidi ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano katika kambi mbili za wakimbizi utafiti ambao uliainishwa kwa kiasi kikubwa kuwa wa chini kuliko ilivyotarajiwa, na kwamba inaaminika robo ya watoto hao walikwisha kufa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni