Bushoke afunguka asema Diamond ni aina ya wasanii wanaotakiwa nchini
Msanii mkongwe wa muziki nchini, Bushoke amemmwagia sifa mkali wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz kuwa ndiye msanii anayetakiwa kuigwa na wasanii wengine.
Muimbaji huyo alisema kuwa Diamond ni miongoni mwa wasanii wa kizazi kipya anaowakubali kwa ufaisi wake wa kazi.
“Diamond ni mwanamuziki ambaye ni mfano wa kuigwa kwa kizazi hiki kwani anajulikana alipotokea, alikuwa anaishi na mama yake mzazi Tandale na sasa ukimzungumzia ni mtu wa kimataifa hata Afrika Kusini amejijengea heshima, wasanii wa hivi ndio wanaotakiwa nchini,” Bushoke aliliambia gazeti la Mwanaspoti.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alisema baadhi ya wasanii wapya wanabebwa na skendo ndio maana wanashindwa kukaa kwenye game kwa muda mrefu.
“Kinachowabeba chipukizi ukiacha wachache wanaofanya kazi ni skendo za kutengeneza na sio ubora wa kazi, kitu ambacho wakongwe hawezi kufanya upuuzi badala ya ukomalia kutoa kazi lakini hawapewi sapoti kubwa,” alisema Bushoke.
Aliongeza,”Muziki wa sasa umetawaliwa na skendo tofauti na miaka mitano nyuma ambapo, wengi wetu tulikuwa tunavuma kwa vipaji na ujumbe uliyomo katika nyimbo, leo ili msanii atoke lazima kwanza ajitangaze kwa skendo tena za mapenzi.”

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni