Kifaa kikubwa cha chuma kimeanguka kutoka angani katika eneo la migodi Kaskazini mwa Myanmar
Kifaa
hicho cha muundo wa mviringo, kilichopatikana siku ya Ijumaa katika
jimbo la Kachin, kina urefu wa mita 4.5 na upana wa mita 1.2.kifaa kingine cha chuma chenye maandishi ya kichina kilitoboa paa la nyumba iliyo karibu wakati mmoja lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Inakisiwa kuwa kisa hicho huenda kinahusiana na satellite ya China iliyorushwa angani.
Wakaazi walisema kuwa walisikia sauti kubwa kabla ya kifaa hicho kuanguka
- Wana anga wawili wa China wafika anga za juu
- Wanasayansi kuunda taifa jipya anga za juu
"Tulishikwa na hofu kwa sababu ya mlipuko huo," mwanakijiji Ko Maung aliliambia gazeti la Myanmar Times.
Vifa hivyo vinaaminiwa kuwa vya satellite au sehemu za injini ya nge au kombora.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni