Mashabiki wa nyota wa filamu za Kichina Bruce Lee wamekosoa filamu mpya ya nyota huyo inayopotosha kuhusu maisha yake.
Filamu
hiyo 'Birth of the Dragon' inaonyesha maisha ya nyota huyo alipokuwa
mdogo nchini Marekani pamoja na pigano lake lililozua utata dhidi ya
bwana Wong Jack Man mwaka 1964.Filamu hiyo ilioelekezwa na George Nolfi ,ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika sherehe ya filamu ya Toronto.
- 'Bruce Lee' achaguliwa kuwa diwani Afrika Kusini
- Jackie Chan kupewa tuzo ya Oscar ya staha
''Huu ni utani? Nilikuwa hapa umuona Bruce Lee,lakini wakati mwingi wamekuwa wakimuonya mtu mmoja mweupe'',aliandika mtumiaji wa IMDb ticklegear katika shambulio la mtanda wa kijamii.
"Badala ya kusherehekea vile Bruce Lee alivyokuwa mnyama ,wamemfanya aonekane mtu muoga na mwenye wivu.Hii ni sawa na kushusha hadhi ya muigizaji huyo badala ya kuonyesha maisha yake''.
Aliongezea: Ni filamu mbaya ,nisingeipendelea kwa sababu inaharibu historia ya Bruce Lee kwa kuongeza uongo mwingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni