Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu anaandaa utaratibu wa kumfikisha
mahakamani aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia
kitendo cha msanii wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Raymond ‘Rayvanny’
kumtumia kwenye video ya wimbo wake wa Natafuta Kiki bila makubaliano.
Akizungumza nasi hivi karibuni, Wema alisema amefikia uamuzi
huo kutokana na Diamond kukiuka makubaliano waliyofanya awali kuhusu
yeye kuonekana kwenye video hiyo. Alisema: “Diamond alinifuata na
kunitaka nionekane kwenye video ya msanii wake Raymond, nikamwambia
anipe milioni 10, yeye akaonesha alikuwa anataka free huku akisema mbona
nilimsaidia Ommy Dimpoz.
“Nilimwambia kuwa nilimsaidia Dimpoz kwa kuwa alikuwa anahitaji msaada
lakini yeye nilitaka anipe kiasi hicho cha pesa. “Baadaye niliongea na
Martin Kadinda kuhusu kile alichotaka Diamond na pesa ambayo nilimtajia,
Martin akaniambia kwa ishu hiyo hata milioni 10 ni ndogo, nikashituka
na ndiyo maana hata Diamond aliponipigia tena kuhusu ishu hiyo
nilimchomolea.” Wema akaendelea kudai kuwa, licha ya kwamba yeye
alishakataa kuonekana kwenye video hiyo, siku ya ‘bethidei’ ya Rommy
Jones alifanyiwa kitendo ambacho si cha haki
“Nikiwa pale kwenye ‘bethidei’ ya Rommy, bila kujua wana lao jambo,
Raymond akawa anajiweka sana kwangu huku video na picha mbalimbali
zikichukuliwa, sikujua kwamba kuna kitu nyuma yake, ile video ilipotoka
nikashangaa nimetumika bila ridhaa yangu.
“Ndiyo maana nimewasiliana na wanasheria wangu ili nimshitaki
Diamond kwani yeye ndiye niliyezungumza naye na tukashindwana,” alisema
Wema. Kufuatia tuhuma hizo, Risasi lilifanya jitihada za kuwatafuta
Diamond na Raymond ili kuzungumzia madai hayo lakini hawakuweza
kupatikana mara moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni