Kurasa

Ijumaa, 23 Septemba 2016

Watuhumiwa wa kuchoma makanisa Kagera wahukumiwa kifungo cha maisha.

Mahakama ya hakimu mkazi Bukoba imewatia hatiani na kuwahukumu kwenda jela kutumia kifungo cha maisha watu watatu ambao ni pamoja na Ngesella Joseph, Rashid Mzee na Ali Dauda waliokuwa na tuhuma ya kuhusika na vitendo vilivyokuwa vimekithiri mkoani Kagera mwaka jana vya uchomaji wa makanisa ya madhehebu ya kikristo katika maeneo mbali mbali ya mkoa huo.

Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Victor Bigambo, akisoma hukumu hiyo amesema mahakama imetoa adhabu hiyo kwa watu hao baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Mwendesha mashtaka wa serikali, Emmanuel Mavelle amesema watu hao mashtaka yaliyowatia hatiani kuwa ni ya kula njama na kuchoma makanisa pia amesema watu hao wanakabiliwa na mashtaka mengine ya kuua watu kwa kuwakata watu makoromeo ambayo yanasikilizwa na mahakama kuu kanda ya Bukoba.

Kamanda wa jeshi la polisi katika mkoa wa Kagera kamishina msaidizi mwandamizi Augustine Ullomi aliyekuwa mahakamani wakati hukumu ikitolewa amewaomba wananchi waendelee kuwafichua waharifu ili jeshi hilo liweze kukabiliana nao.
Chanzo:Muungwana.co.tz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni