Kesi dhidi ya wanawake watatu walioshukiwa kuhusika katika shambulio
dhidi ya kituo kimoja cha polisi katika mji wa bandarini wa Mombasa
nchini Kenya mwishoni mwa juma, ilishindwa kufanyika kutokana na
matatizo ya mawasiliano.
Mmoja wa washukiwa hafahamu kabisa Kiingereza au Kiswahili.
Shukri Ali, ambaye ni mlemavu wa kutosikia, hakujibu lolote hata baada
ya mfasiri wa ishara aliyeletwa mahakamani kumsaidia kuelewa kesi dhidi
yake.
Mtafsiri wa lugha ya Kisomali pia alikuwa mahakamani ili kuwasaidia
washukiwa wawili, Saida Ali na Naima Mohamed Ali, ambao hawana uwezo wa
kufahamu Kiingereza.
Jaji Emmanuel Mutunga, aliamuru Shukri Ali, kupelekwa hadi katika
wachunguzi maalum wa kimatibabu, katika hospitali ya kitaifa ya Coast
General.
Wanawake hao watatu, ambao bado wanazuiliwa pia watachunguzwa na madaktari.
Wanashtakiwa kwa kosa la kuwapa hifadhi wanawake watatu wanaodaiwa
kuunga mkono kundi la Islamic State, ambao waliuwawa pale walipojaribu
kushambulia kituo cyha polisi cha Mombasa siku ya Jumapili iliyopita.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21, wakati ripoti ya kimatibabu itakapowasilishwa mahakamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni