Mkurugenzi Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel
akizungumza katika semina ya wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia
kuondoka kesho kwenda vyuo vikuu vya nchini China, iliyofanyika katika
ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wanaokwenda nje wakichukua tiketi pamoja na viza kwa ajili ya
safari kwenda katika vyuo vikuu vya nchini China iliyofanyika jijini
Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi na wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Globa
Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel hayupo pichani katika semina
iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
MKURUGENZI Mtendaji wa Globa Education Link (GEL), Abdulmaalik
Mollel amesema wanafunzi wanaokwenda nje waliohitimu masomo katika vyuo
vya nje wanatakiwa watafutwe na waajiri na sio wawe wa kutafuta ajira.
Mollel ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina na
wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka kesho katika vyuo vikuu
vya nchini China, amesema kuwa kutokana na vyuo hivyo kuwa na vifaa vya
kujifunzia wanafunzi wakitumia vizuri katika soko la ajira watatafutwa.
Mollel amesema nchi haina tatizo la ajira hivyo watu wanatakiwa kuwa na
uwezo binafsi ambao utamfanya mwajiri kutafuta mtu wa kumuajiri hivyo
wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo wanatakiwa kutumia maarifa ya kuja
kuzalisha nchini.
Amesema wazazi watumie muda wao katika kuwafuatilia watoto wao wanaosoma
nje ili kuweza kuona thamani ya fedha wanazozitoa na elimu wanayoipata.
Aidha amesema kuwa wale ambao wanahitaji vyuo vya nje bado nafasi zipo
na wanafunzi wote watafuata taratibu zote ikiwa ni pamoja Tume ya Vyuo
Vikuu nchini kujiridhisha na vyuo wanavyokwenda. Mollel amesema
haitakuwa tayari kuona wanafunzi wanahitimu vyuo vya nje kupitia GEL
kuwa hawatambuliki.
Chanzo: Muungwana blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni