Kurasa

Ijumaa, 16 Septemba 2016

Walimu Wakuu wa Mashule Mbali mbali Nchini Tanzania Kuanza Kuneemeka:

 

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa

Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5.09 kwa ajili ya kutoa posho ya motisha ya madaraka kwa walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu elimu kata ili kuwa na usimamizi mzuri wa sera ya elimu bure ili iweze kuleta tija kwa taifa.
Hayo yamezungumzwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa kwenye hotuba yake ya kuahirisha bunge iliyokuwa inazungumzia mambo mbalimbali ya kiserikali na shughuli za bunge.

Waziri Majaliwa amesema kuwa serikali imeanza kutoa pikipiki kwa waratibu elimu kata kila mkoa nchini ili ziwawezeshe katika ufatiliaji na usimamizi wa shughuli za kielimu katika kata zao nchi nzima.

Waziri Majaliwa amesema kuwa kwa kuanzia tayari waratibu kata wa mikoa 7 ambayo ilikuwa na ufaulu wa chini katika matoke ya kuhitimu darasa la saba na tayari wameshapatiwa jumla ya pikipiki 1015.

Aliitaja mikoa hiyo iliyopata pikipiki hizo ni pamoja na Mkoa wa Dodoma, pikipiki 192,mkoa wa Mara 99, Simiyu 122, Shinyanga 128, Tabora 200, Kigoma 135 na Lindi Pikipiki 139.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema kuwa katika kukabiliana na upungufu wa walimu serikali imeamua walimu watakaoajiriwa mwaka 2016 wapangwe shuleni moja kwa moja na kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa walimu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni