Ilipoishia...
“nani kachanganyikiwa”
Nilishindwa kuvumilia ikanibudi nizungumze,taratibu nikiwa ninashuka kwenye ngazi na mkononi nikiwa nimeshika bastola na kuwafanya mama na sheila kustuka
Endelea.....
Sheila kwa haraka akarudi nyuma ya mama na kujificha,mama akanitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao
“eddy mwanangu unataka kufanya nini?”
“nataka kujua huyu mwanamke kwa nini amesema kuwa mimi nimechanganyikiwa”
“hujachanganyikiwa mwanangu,tulikuwa tunazungumza kuhusiana na baba yako mzee godwin kwamba amechanganyikiwa”
“mama na wewe unashiriki zambi ya uongo?”
“kweli mwanangu,aliniambia kuwa amemuona sehemu fulani katikati ya jiji akiwa anaruka ruka”
Nikamtazama mama kisha nikakaa kwenye sofa na kuiweka bastola pembeni yangu.Sheila akabaki akinitazama huku akiwa hana la kuzungumza.Wote wakaka na kunitazama,ukimya ukatawala ndani ya dakika kadhaa mama akaamua kuuvunja ukimya.
“eddy na hiyo bastola yangu unakwenda nayo wapi?”
“kuna kazi ninataka kwenda kuifanya”
“eddy mwanangu,hembu niambie ni nini tatizo linalo pelekea kuwa na roho kama hiyo kwa maana umerudi hujazungumza na mimi vitu vingi zaidi ya kwenda kulala?”
“mama bado mimi nipo,tutazaungumza kila kitu”
“sawa,ila kwanini ume......”
Nikauona mguu wa rahma ukiukanyaga mguu wa mama na kumfanya asiimalizie sentesi yake.
“kwa nini umekaa huko mbali pasipo kuwa kunijulisha?”
“huyo hajakuambia?”
“yeye atajuaje mtoto wa watu?”
“ahaa mama hiyo mada tutazungumza kesho.Oya ninaomba funguo”
“za nini?”
Sheila alizungumza kwa sauti ya upole na yenye unyeyekevu mkubwa
“funguo za gari na nyumba yako.”
Sheila akafungua pochi yake na kunipa.
“mbona umevaa nguo hizo hizo ulizo kuja nazo?”
Nikajitazama kuanzia chini hadi juu,nikarudi chumbani kwangu na kuvaa nguo zangu vizuri,nikaichomeka bastola kiunoni mwangu na kuifunika na tisheti nyeusi niliyo ivaa,nikurudi sebleni.
“wewe twende basi home”
Sheila akatazama na mama kisha akanitazama na mimi
“mmmm nitalala na mama”
“hutaki au?”
“eddy muache mwenzako alale hapa,kwani huku kwake unakwenda kufanya nini?”
“kulala”
Nikataka kutoka na mama akaniita
“bastola yangu ipo wapi?”
“nimeirudisha”
“wapi?”
“kwani mama ilikuwa wapi?”
“basi baba nenda salama”
Nikatoka na kuufunga mlango vizuri.Nikasimama pembeni ya dirisha na kusikilizia ni nini mama na sheila watakizungumza,kwa kupitia uwazi ulioachwa na dirisha nikawaona wakikaa kwenye sofa
“mbona mwanangu amebadilika namna hii?”
“mama wee acha tuu,eddy mimi ninampenda ila kwa hapa alipo fikia ninamuogopa mama”
“mmmm usimuogope”
“mama eddy kuna kipindi alipokuwa na hasira mimi nilikuwa nikimtuliza na kumsogelea,ila sasa hivi mmmmmm ni bora nimtoroke toroke hadi atakapo kaa sawa”
“itabidi nitafute madaktari watakao muhudumia”
“ni kweli mama,yaani mtu anazungumza kwa sauti nzito kama simba dume”
“ila mwanangu huyu anaugonjwa wa asira,mimi wala simshangai sana kwani kuna kipindi akiwa mdogo alisha wahi kumuua mwenzake shule kwa kumpiga na chupa ya soda kichwani”
“weeeee?”
“ooohhh ilikuwa ni kesi kubwa kilicho muokoa ni udogo wake kwa alikuwa na miaka mitano”
“mama ina maana eddy kuua hakuanza leo?”
“eddy mwangu akiwa na hasira si mtu wa kumsogelea,nilisha mpeleka hadi kwa wachungaji wamuombee ila wapii.Nilijaribu kutafuta wana saikology labda wakae nao ila imeshindikana.Kila dawa ambayo niliambiwa inafaa kwa kipindi hicho kuwa kama kitulizo cha ugonjwa wake ila wapi?”
“mmmm”
“yaani na haya matatizo yaliyo tokea hichi kipindi cha hivi karibuni naona pia yanachangia sana”
Nikataka kuondoka niwahi ninapotaka kwenda ila swali la sheila likanifanya nipige hatua kadhaa kurudi dirishani
“kweli mama,hivi mzee godwin yupo wapi?”
“hadi leo sijamuona,mimi mwenyewe ninafanya uchunguzi nije kumuona ila hadi sasa hivi sijapata jibu”
“mama tutasaidiana katika hilo,yule mzee ni muuaji sana”
Sikuona haja ya kuendelea kusikiliza mazungumzo yao zaidi ya mimi kuondoka,nikaingia ndani ya gari na mlinzi akanifungulia geti na kuondoka,nikafika kwenye kituo cha kuongeza mafuta.Nikajaza tanki la gari na kulipa kiasi ambacho kimegharimu kiasi hicho cha mafuta.
Njia
nzima nikawa ninafikiria ni wapi alipo mzee godwin.Nikafika nyumbani
kwa sheila na kushuka kwenye gari na kufungua geti,nikaliingiza gari
ndani na kufunga geti.Nikafungua ndani na kuchukua kirimoti cha
kufungulia sehemu ya kuifadhia gari,nikaingia na kuchukua turubai lenye
mwili wa derick ambao niliubanika vizuri
Nikauingiza ndani ya buti la gari na kulifunga vizuri,nikafunga kila sehemu kama nilivyo iacha,kabla sijatoka nikakumbuka simu ya derick niliiacha sofa nikiwa nimeizima,nikaingia ndani na kuichukua ila sikuiwasha,nikafungua geti na kutoa gari.Nikarudi kulifunga na safari ya kuelekea arusha ikaanza,kutokana ni usiku sana hapana magari mengi zaidi ya maroli ya mizig ambayo yanakwenda kwa kasi na usipo kuwa makini utajikuta ukigongwa.
Nikazidi
kuongeza mwendo na kimoyo moyo nikawa na kazi ya kumuomba mungu
nisipate ajali kwani mwendo ninao tembea nao endapo nitakubwa hata na
baiskeli basi kitakaocho endelea kwenye kuanguka nahisi kitakuwa ni kifo
tu.Kwa hofu nikapunguza mwendo kutoka spidi 250 hadi mia moja japo gari
bado ipo kwenye mwendo mkali sana.
Mwanga mkali wa gari linalokuja nyuma yangu ukaanza kuniumiza macho,nikapunguza mwendo na kumuwashia taa nikimuashiria apite kwani sikuweza kuendesha kwa jinsi taa zake zinavyo niumiza macho kupitia vioo vya pembeni.Nikashuhudia gari aina ya ‘hammer’ yenye rangi nyeusi na vioo vyake vyote vikiwa ni vyeusi na limefungwa likinipita,haikuwa ni moja zikapita nyingine mbili zikiwa katika kwendo kama ilivyo gari ya kwanza
“mmmmmm ni kina nani hawa?”
Nilijiuliza maswali,na mimi nikaanza kuongeza mwendo wa gari langu.Jinsigari hizi zinavyozidi kwenda ndivyo nami nilivyodidi kuongeza mwendo,nikaanza kuzikaribia kwa karibu.Nikawasha taa zote za gari langu ili na mimi nimtese dereva wa gari la nyuma.Nikashanga kuona gari mbili za nyuma zikitanda barabarani na kunizuia kupita.Nikaanza kupatwa na mashaka baada ya madereva hao kuanza mtindo wa kupunguza punguza mwendo gafla gafla na usipo kuwa makini unazigonga kwa nyuma.
Kwa mbele likawa linakuja lori ikatulazimu sote kubana upande mmoja kuliacha lipite na mchezo ukarudi na kuwa wa kuzuiana kupita.Hadi tunafika daraja la wami ndio gari hizo zikapunguza mwendo kulikwepa fuso lililo haribika pembezoni mwa barabara
Tukalimaliza daraja,nikaona jamaa wananichelewesha nikamuomba dereva wa nyuma kuweza kupita akaniruhusu,nikiwa ninamaliza kuliacha gari la nyuma gari la pili kutoka mbele likatanda barabarani na kuongeza mwendo.Dereva wa gari la nyuma akaongeza kasi zaid na kutanda kwa nyuma wakawa wameniweka katikati.Kwenye kioo kidogo kilichopo pembeni ya mskani kwenye gari langu nikaanza kuwaka taa nyekundu na kutoa maandishi yaliyo andikwa kwa herufi kubwa.
{habari yako bwana eddy,gari yako ipo kwenye wakati mgumu wa usalama.Kama unataka ulinzi minya hapa au unaweza kukata}
Nikaminya sehemu yenye alama ya tiki(pato).Sikushangaa sana kwa maana hili gari aina ya bmw 007 limetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na ninakumbuka sheila aliniambia kwamba amepewa na wamarekani weusi alio cheza nao filamu ya ngono.Gari ikaanza kurudi chini kidogo kisha vioo vyote kasoro cha mbele vikapitiwa na ukungu mweusi ambao sikujua ni wa nini.
Kwenye kioo kidogo nikaona gari la mbele na la nyuma,nikaonyeshwa jinsi zivyo ndani na idadi ya watu waliomo ndani wakiwa katika hali ya mifupa(mafuvu).Nikiwa ninashangaa shangaa nikastukia nikigongwa na gari ya nyuma na kunifanya nishindwe kulizuia gari na likamgonga gari la mbele.
Nikastukia kuona jamaa wawili kwenye gari la mbele wakichomoza kwenye vioo vya pembeni na kuanza kunishambulia kwa kutumia bunduki zao,kitu kilicho nistaajabisha ni jinsi risasi hizo kushindwa kuingia ndani ya gari langu.Nikaanza kujiamini kuwa gari yangu imepata kweli ulizi,nikakanyaga breki za gafla na kusababisha gari la nyuma kunigonga na kuanza kuzunguka barabarani kwa kasi na kuacha njia na kuvaamiti iliyopo pembezoni mwa barabara na kupinduka.
Nikaachia
breki na kulifukuzia gari la mbele ambalo kidogo liliniacha kutokana na
mwendo wao wa kasi,nikalisogelea kwa ukaribu,kila ninapo jaribu
kulipita wananizuia.Nikaongeza mwendo,kutokana na gari yangu kuwa chini
kidogo likaweza kupiga tairi za nyuma na kulifanya linyanyuke kidogo na
dereva wake kushindwa kulimudu na kuanguka vibaya na kuanza kubingirika
likiingia msituni.
Gari la mbele likapunguza mwendo na kutokana lipo mbali kidogo na mimi, likafunga breki za nguvu na kwa utaalamu mkubwa dereva wa gari hilo aliweza kuligeuza na likawa limegeuka nilipo mimi.Nikapunguza mwendo hadi nikasimama mita chache kutoka lilipo gari langu.Derevaa wa gari lililopo mbele yangu akaanza kuvuta mafuta huku akiganyaga breki na kuzifanya tairi za gari lake kuzunguka kwenye lami pasipo kwenda mbele na kuzifanya zitoe mlio fulani.Nikazima taa za gari langu na dereva akazima za kwake.Nikawasha za kwangu ila nikajikuta nikinshangaa dereva wa gari hilo kwani anafanana sana na manka japo simuoni vizuri ndani ya gari hilo.
Gafla
nikalishuhudia roli linalo malizia kona iliyopo karibu na lilipo simama
‘hammer’,sikujua kama dereva wa hammer ninaye mfananisha na manka kama
ameliona lori hilo au la kwani anaendelea kuzifunga breki za gari lake
katikati.Nikazisika honi za lori zikimuashiria dereva wa hammer kuondoka
barabarani,ndani ya sekunde kadhaa nikastukia kuona lori likiligonga
kwa nyuma hammer na kulisogeza pembeni ya barabara na lori likapita
pasipo kusimama.
Ukimya ukatawala kesemu nzima,nikataka kuondoka ila nikataka kujua niliye muona ni manka kweli au sio yeye.Nikalisimamisha gari pembeni,nikaichomoa bastola yangu,nikafungua mlango na kushuka ndani ya gari.Nikatazama pande zote za barabara hapakuwa na gari lolote linalo kuja.Nikaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari hadi sehemu lilipo anguka gari la watu ambao ninahisi sio watu wazuri.Nikalisogelea taratibu.Nikachunguza ndani na kumuona mtu moja aliye kaa pembezoni mwa dereva akiwa amekitwa na kisiki cha mti kwenye kichwa na amefariki hapo hapo,siti za nyuma zilijaa maboksi makubwa na hapakuwa na mtu wa aina yoyote.
Dereva
wa gari ambaye ni mwanamke aliendelea kujitahidi kutoka ndani ya gari
pasipo kugungua kama mimi nipo eneo hilo.Akasimama huku nywele zake
nyingi zikiwa zimemfunika usoni mwake,akakutana na mdomo wabastola
yangu.Akajiweka nywele vizuri na nikahakikisha ni manka kwani akawa ni
wakwanza kuliita jina langu
“eddy”
“naam”
“eddy”
“naam”
Tukakosa cha kuzungumza,uvaaji wa manka unaashiria kuwa ni jambazi kwani kuanzia juu hadi chini amevaa nguo nyeusi tupu zinazo endana na nguo za jeshi.Mikono yake amevaa gloves nyeusi.Kifuani amejifunga jaketi la kuzuia risasi(bullet proof).Kiunoni mwake anabastola mbili zilizo chomekwa kwa kwenye kiuno
“umeumia?”
“hapana”
“tuondoke”
“hapana ngoja kuna kitu tusaidiane”
“nini?”
“kutatoa haya maboksi”
Sikutaka kuuliza yana nini zaidi ya kusaidiana kwa pamoja kuyatao maboksi mawili makubwa kiasi.Kwa uzuri yakaingia kwenye gari langu siti ya nyuma.Manka akachomoa bastola yake na akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kuftatua risasi kazaa kwenye tanki la mafuta ya gari lao na likalipuka.Akaingia ndani ya gari langu na safari ikaendelea.Dakika kumi nzima ndani ya gari hakuna aliye msemesha mwenzake.
“eddy usiku huu unakwenda wapi?”
“arusha”
“kuna nini?”
“kuna ishu ninakwenda kufanya na wewe je?”
“nitakuambia tukitulia”
“boksi zina nini?”
“pesa”
“pesa.....!!?”
“ndio”
“za nani?”
“ndio maana ninakuambia nitakuambia tukitulia”
Nikazidi kuongeza mwendo na ndani ya masaa mawili tukawa tumefika arusha.Tukafika hadi kwenye mtaa wa wachaga na tukaingia kwenye moja ya nyumba iliyo tulia sana.Manka akashuka kwenye gari na kufungua geti na mimi nikaliingiza gari ndani akafunga huku akitazama pande zote kisha akalifunga geti.Akafungua mlango wa nyumba hiyo na tukayaingiza maboksi yote ndani.Tayari mwanga wa jua ulisha anza kuchomoza kwa mbali ikiashiria ni asubuhi.
“oya mimi ngoja nikapige mishe ninayo itaka kisha nitakustua”
Nilimuambia manka ambaye alianza kukata biksi moja kwa kutumia kisu.Nikashuhudia vibunda vya elfu kumi kumi vikiwa vimejaa ndani ya boksi
“nimeshatoka kimaisha mpenzi”
“mmmm....”
Manka akanirushi kibunda kimoja cha pesa kuku vingine akivitoa na kuvirusha rusha juu kwa furaha.Manka akanifwata na kunikumbatia kwa furaha huku akinipiga mabusu mdomoni
“eddy furaha yangu imekamilika sasa”
“kwa nini?”
“nina pesa na nimekupata wewe,nilikutafuta kwa siku nyingi mpenzi wangu”
Wazo la manka kuwa ni dada yangu likanijia akilini mwangu.Nilipo kumbuka kuwa baba yake ni baba mkubwa nikakaa kimya pasipo kujibu chochote.
“nikupeleke sehemu ambayo unataka kwenda?”
“hapana”
“twendwe wote bwana”
“ila ubadilishe nguo zako”
“unadhani sina akili,nilazima nibadilishe”
Manka akaniachia na kuingia kwenye moja ya chumba.Baada ya muda akatoka akiwa amejiremba na mtu unaweza kumsahau kama yeye ndie aliyekuwa akiliendesha gari la majambazi.Nikalitoa gari nje,akafunga geti lake,akaingia ndani ya gari nasafari ikaanza.Nikalisimamisha gari nje ya geti la madam mery
“hapa kama napajua?”
“ni kwa mwalimu wangu mmoja”
“namjua si yule mery?”
“ndio,ila nisaidie kitu”
“kitu gani?”
“ninaomba ukagonge”
“alafu”
Nataka kuingiza gari humo ndani”
Manka akashuka kwenye gari na kuaza kugonga geti,dakika kama mbili gati likafunguliwa na madam mery.Wakasimuliana kwa furaha na madam mery.Kutokana na kufunga vioo vya gari langu madam mery hakuweza kuniona.Madam mery akazungumza kidogo na manka kisha akafungua geti na manka akarudi ndani ya gari.
Endelea nayo kupitia, Ubuyublog.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni