Kurasa

Jumanne, 13 Septemba 2016

Pluijm ampa 'Big Up' Mahadhi

 


KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm amesifu kiwango cha kiungo wa pembeni Juma Mahadhi na kusema kuwa ni aina ya wachezaji anaowakubali na amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi chake.

Pluijm, ambaye mara nyingi hapendi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja kwenye kikosi chake, lakini mwishoni mwa wiki alishindwa kujizuia na kudai kuwa Mahadhi amekuwa akicheza kwa kasi, na kuhaha uwanjani huku na kule kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Katika mchezo wa Yanga na Majimaji uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mahadhi aliingia kipindi cha pili akitokea benchi akichukua nafasi ya Obrey Chirwa na kufanikiwa kuiwezesha timu yake kufuanga mabao 3-0 dhidi ya Majimaji.

“Mahadhi kwangu ni ‘Super Sub’ washambuliaji wangu walipoteza nafasi nyingi na walikosa umakini, lakini alipoingia Mahadhi alibadili mchezo, alicheza kwa kasi na kupeleka mashambulizi zaidi kwa wapinzani ndio uchezaji ninaouhitaji,”alisema Pluijm huku akiangua kicheko cha furaha.

Pluijm alisema aina ya uchezaji wa Mahadhi, inamshawishi kocha kumpa nafasi ya kucheza hata kama imebaki dakika moja kabla ya mchezo kumalizika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni