Wakati wewe unawaza ni lini utaweza kuimiliki shilingi milioni 2 ili
kufanyia mambo yako ya msingi, huko Ulaya, kuna watu waliopiga kambi
siku mbili kusubiria kununua simu mpya, iPhone 7 iliyoingia sokoni
Ijumaa hii.
Mistari mirefu imeonekana katika baadhi ya nchi 28 duniani ambako simu hiyo imeanza kuuzwa.
Baadhi ya mashabiki waliweka kambi nje ya maduka ya Apple kwa siku
kadhaa huko Sydney, Hong Kong na Tokyo wakisubiri kuanza kuuzwa kwa simu
hizo.
Bei zake si haba –iPhone 7 inauzwa kwa $1079 (zaidi ya shilingi milioni
2.3) na iPhone 7 Plus ni $1279 (zaidi ya shilingi milioni 2.8).
Tazama picha zaidi:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni