Mwandishi mmoja wa mjini mjini New Orleans alikimbia na kuingia ndani ya nyumba yake iliyokuwa inateketea, kuokoa laptop yake iliyokuwa na vitabu vyake viwili vya riwaya ambavyo alikuwa amekamilisha kuviandika.
"Mtu yeyote ambaye amewahi kutengeneza kazi ya sanaa (anaweza kuelewa), huwezi kupata vingine," Gideon Hodge, 35, aliambia gazeti la The New Orleans Advocate.
Alinusurika kuondoka kutoka kwenye nyumba hiyo salama pamoja akiwa na kompyuta hiyo.
Hakupata majeraha yoyote.
"Laptop hii ina kazi ya maisha yangu yote," anasema Hodge.
Anajieleza kama mtunzi wa michezo ya kuigiza, mwandishi wa riwaya na mwigizaji.
"Moto huo ungekuwa mbaya zaidi," mkuu wa wazima moto wa New Orleans Timothy McConnell, anasema.
Edderin Williams, 38, mkazi mwingine, alifanikiwa kuokoa kipochi chake na funguo lakini hakufanikiwa kuokoa kitu kingine chochote.
Unapogundua moto umezuka kwenye nyumba, serikali ya Uingereza inawashauri watu "kutulia na kuchukua hatua upesi" na kuhakikisha "kila mtu ameondokea kutoka kwenye jumba haraka iwezekanavyo."
Aidha: "Usipoteze muda kuchunguza nini kinafanyika au kuokoa vitu vya thamani."
Chanzo: bbcswahili.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni