Kurasa

Jumamosi, 17 Septemba 2016

Mtoto asaidiwa kufa nchini Ubelgiji

Ubelgiji ni nchi pekee duniani, ambayo inaruhusu mtoto wa umri wowote ule, kuamua kama anataka kufa. 
 Ubelgiji ni nchi pekee duniani, ambayo inaruhusu mtoto wa umri wowote ule, kuamua kama anataka kufa.

Mtoto mmoja nchini Ubelgiji amesaidiwa kufa, kikiwa ndicho kisa cha kwanza cha aina hiyo, tangu sheria kupitishwa kuruhusu watoto wanaoteseka na ugonjwa usiotibika, kuomba waruhusiwe kufa.
Mwenyekiti wa bodi inayosimamia utaratibu huo, uitwao euthanasia kwa Kizungu, Wim Distelmans, alisema kisa hicho kiliripotiwa na daktari mmoja juma lilopita.

Alisema mtoto huyo alikuwa mahatuti, lakini hakutaja umri wala jinsia yake.

Mwanariadha mlemavu wa ubelgiji Marieke Vervoort anayeugua ugonwa usiotibika naye anasema ataomba kufa atakapofanya uamuzi
Mwanariadha mlemavu wa ubelgiji Marieke Vervoort anayeugua ugonwa usiotibika naye anasema ataomba kufa atakapofanya uamuzi

Ubelgiji ni nchi pekee duniani, ambayo inaruhusu mtoto wa umri wowote ule, kuamua kama anataka kufa.

Sheria hiyo iliyopitishwa Februari, mwaka wa 2014, imezusha mjadala nchini na sehemu nyengine za dunia.

Nchini Uholanzi ni mtoto wa umri wa zaidi ya miaka 12 ndio anaruhusiwa kuamua kufa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni